Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2020

IN THE NAME OF JESUS I PUNCH MY ENEMY WITH UPPERCUT.

IN THE NAME OF JESUS I PUNCH MY ENEMY WITH UPPERCUT (Nilikua mcheza Ngumi/Bondia- uppercut ni ngumi mbaya unamchimba adui akiinama kutoka chini kuja juu.sasa huyu anaomba anampiga adui hii ngumi).IN THE NAME OF JESUS I PUT MY ENENEMY IN THE COFFIN(anaomba anamuweka adui yake ndani ya jeneza maana yake afe ) SISI MAOMBI YETU SIO YA KUUA, BALI TUNAOMBEA MABAYA ALIYOKUSUDIA ADUI YASITUPATE.USIOMBE HIVI-MFANO UNAOMBA UNASEMA "BWANA NAKUSIHI ADUI FULANI USIMWACHE, UNAKUMBUSHA UNASEMA BWANA UMESEMA WEWE NDIYE ULIPAYE KISASI TENDA BWANA, TENDA BWANA(yaani ampige adui yako) USIFANYE HIVYO KABISA HAUTAKUWA MTOTO WA MUNGU. KANUNI MOJA YA KUWA MTOTO MUNGU NI KUWAPENDA ADUI KAMA NENO LINAVYOSEMA.KWA HIYO UKIMPENDA ADUI HUWEZI KUMUOMBEA MABAYA AU KUKUMBUSHIA HASIRA YA MUNGU JUU YA ADUI.UKIONA MAOMBI YAKO NI YAKUMKUMBUSHA MUNGU KUMPIGA ADUI UJUE UPENDO HAUPO NDANI YAKO, NA KAMA HUNA UPENDO UJUE HUNA MUNGU.MUNGU NI UPENDO, KAMA HAMNA UPENDO HAMNA MUNGU. STEFANO ALIPIGWA NA MAWE KIMWILI N...

Usiwe Mti unao haribu Ardhi.

Binadamu aliyefanikiwa ni mtu ambaye ni msaada katika jamii iliyomzunguka. Mtu wa namna hii anafananishwa na Mti unaozaa matunda. Katika jamii zetu kuna makundi mbali mbali yanahitaji msaada, sehemu nyingine sio fedha ni mawazo tu na kuwatia moyo. Hatari ni hii-kama wewe ni mtu mzuri wa maadili, unajilinda sana/msafi sana, hutendi dhambi, ila unajiishia mwenyewe na familia yako, husaidii watu wenye shida unafananishwa na mti ambao upo lakini hauzai matunda. Hatari ni kwamba unaonekana ni mti ambao unabana nafasi na pia unaharibu ardhi. (LUKA 13:7 Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu?) Binadamu ni mfanao wa miti ya aina tatu. -Mti wa kwanza ni ule unaozaa matunda mazuri (yaani huyu ni yule mtu ambaye hatendi dhambi ni msafi na anasaidia jamii iliyomzunguka, watu wanafaidika kutoka kwake. Huyu ana Heri)   -Mti wa pili ni ule unaozaa matunda mabaya...

Wewe ni Mti bora - Imarisha hapa.

Binadamu hufananishwa na mti wa matunda. Hivyo binadamu anatakiwa azae matunda mazuri. Matunda ni kitu ambacho huchumwa na kumnufaisha mchumaji. Matunda yanayozungumziwa hapa ni tabia njema/matendo ya kumpendeza Mungu na pia matendo ya kuwapendeza wanadamu na kunufaika kutokana na wewe.Jiulize tabia zako ni njema kwa Mungu na watu wanaokuzunguka, watu wanasemaje kuhusu wewe.Jina lako likitajwa mbele za watu huona matunda gani kwako/au picha gani ya haraka hutokea kwao (mfano mwizi, Malaya, tapeli, mkali, muongo, mgomvi, msengenyaji, mchafu, mlevi/cha pombe, mzushi, mpole, mwaminifu, mchapaka kazi, mtenda haki, ana upendo n.k). Pia jiulize watu wanaokuzunguka (jirani zako, serikali yako ya mtaa, familia na ndungu zako n.k) wanafaidika na nini kutoka kwako maana tunda lazima pia limfaidishe mtu wa upande wa pili. Au wewe ndio umekua chanzo cha migogoro na kutia hasara katika familia, kazi, ukoo, mtaa, vikundi n.k. Basi Rafiki yangu kama uko kundi baya badi...

Kuweka wazi udhaifu wa mtu mwingine.

Sifa moja ya mtu mwema/mwenye haki ni kutoweka wazi udhaifu wa mwingine.kutosengenya na kutunza siri za mtu ambazo zikisikika zitamuaibisha muhusika. (MATHAYO 1:19 Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri). Hapa Yusufu aligundua mchumba wake ana mimba ambayo yeye hausiki. akapanga kumuacha kwa siri bila ya mtu mwingine kujua. Sasa jipime kama wewe una tabia ya kusengenya na kupenda kuweka wazi udhaifu wa mtu mwingine au la, kama una tabia hiyo jirekebishe rafiki yangu.   pia jihadhari na watu wanao weka wazi udhaifu wa wengine, wala hakuna umuhimu wa mtu mwingine kujua udhaifu huo.watu wa jinsi hiyo wanamapungufu, warekebishe au wakwepe.

Usifanye dhambi makusudi na kutegemea kutubu ni Hatari.

WAEBRANIA 10:26-27 26 Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; 27 bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao. WAEBRANIA 6:4-6 4 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, 5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, 6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri. Rafiki yangu usitende dhambi kwa makusudi alafu ukasema nitarudi kutubu ni Hatari, Mungu atakuacha bila kujijua. Hapo nyuma ulitenda dhambi kwa makusudi na kwenda kutubu, Mungu amekusamehe kwa sababu ulikuwa ujafunuliwa neno hili, sasa leo amenena nawe ana kwa ana kupitia neno lake kwa hiyo usirudie tena mchezo huo ni hatari sana. Mungu ni mkali kwenye dhambi, hapendi dhambi anaweza...

Faida za kulea watoto mliowazaa na msio wazaa, wajomba, mashangazi, wajukuu, wadogo zenu, wazazi wenu,baba na mama wadogo, bibi babu n.k

WAKOLOSAI 3:23-24 23 Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, 24 mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo. Nakushauri walee watu hao kwa moyo wako wote kama unamfanyia mungu na si unamfanyia mwingine aliyepaswa kulea, kwani kuna baraka nyingi sana.wewe jaribu kuwalea kwa moyo wote utaanza kuona baraka endelevu zikimwagika juu yako, jinsi unavyo kaa nao nawe ndio jinsi mvua ya baraka inavyoendelea kukunyeshea.wape mahitaji wanayostahili kama; vitanda vizuri, mablanket mazuri na mazito, chakula cha kutosha, nguo, viatu n.k wewe jiachie kwao kwani ukiwalea kwa shingo upande huwezi kupata thawabu, miaka yooote ulio kaa nao itakua bure, itakua hasara. Kumbuka wahitaji hao wanaweza kukutendea mabaya, kama kukusengenya, manung’uniko, kutokukutii vyema, kukuibia n.k wewe usiangalia hayo, samehe na endelea kuwahudumia ipasavyo. aloooo kwa kufanya vyema hivyo tegemea baraka za hali ya juu.

Siri ya kukupelekea kufurahia/kuenjoy Maisha.

KUWA NA SIKU NJEMA 1 PETRO 3:10-11 Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila. 11 Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana. -Hii ni kanuni ya kufanya malengo yako ya siku yafanikiwe.Bila kufuata kanuni hiyo maana siku hiyo haitakua njema bali mbaya kama kupoteza vitu, kuibiwa,kuumia,kuugua,kufukuzwa kazi,kupigana,kugombana,kutouza bidhaa, kutokua na amani,kupigwa na kichaa,kuangukiwa na mti/ukuta, yaani kuwa na nuksi kwa ujumla.Kwa kufuata kanuni hizo za mistari hii miwili, utapenda maisha/utaenjoy maisha (ndio maana anasema atakaye kupenda maisha .....) kwa hiyo mtu ambaye hufuati kanuni hii hufurahii maisha, badilika sasa ili zije nyakati za burudani. Maisha yako chini yako. Neno hili linatuangazia kuwa kuifanya siku kuwa njema/maisha mema kupo chini ya uwezo wako. Tumeona moja ya siri ya kuwa na siku/maisha mema ni kuzuia ulimi usinene mabaya. Ulimi kunena mabaya ni kutukana...

Ulimi wako una nguvu, unaharibu hapa.

Methali 15:4 “Ulimi safi ni mti wa uzima; Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo”. Maana yake ulimi wako ukiongea huku ukiwa na asili ya faraja basi unayeongea nae utampa uzima yaani kubadilika kutoka njia mbaya kwenda njia nzuri. Biblia ya kiingereza ulimi safi inaita comforting tongue/yaani ulimi wa kutia moyo/kufariji. Zingatia katika lolote unalomwambia mtu ulimi wako uwe na munyu huu wa faraja/comforting, aah utaponya wengi.Kinyume chake utawavunja moyo wengi na kuua wengi.Unapoongea,kufundisha HAKIKISHA unaongea huku ukiwa na UPENDO, kwa kufanya hivyo utajikuta maongezi, mafundisho yako yanayotoka ulimini mwako yanakua na faraja/kutia moyo na kupelekea mtu kupata uzima katika eneo lililokufa au linalotaka kufa. Tumia njia hii; -unapofudisha mtoto wako. -katika mazungumzo,maeleweshano mume na mke. -mchungaji ukihubiri kama hutumii njia hii utashangaa waumini wanakufa, wanakufa hata kama ni neno la Mungu.Mafundisho yako usimpanie mtu, fundisha kwa upendo. -tumia comfo...

Tambua kusudi lako Duniani.

BINADAMU umeumbwa kwa KUSUDI fulani dunia. Ila wengi hawajui KUSUDI sahihi. Jibu ni (Mathayo 5:14a Ninyi ni nuru ya ulimwengu).Hilo ndio KUSUDI lako, wewe umeninginizwa kama bulb/taa, kama jua, watu waone matendo yako mema,pia uwamulikie walio potea waone njia. Pia Kuhusu KUSUDI ulilopangiwa kiuchumi la kukuwezesha kuishi duniani ni kwamba ;lazima utajikuta kuna kitu unakiweza, kitu hicho kiendeleze shuleni. Pia mwingine utajifunza kitu kipya kabisa kutoka shuleni huku amani yako ikiwa inakubaliana nacho. (Mithali 4:13 Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako) Lazima unapochagua masomo utaona amani yako inakubaliana na masomo hayo jua ilo ndio kusudi lako liendeleze.Mtoto wako muelekeze umuhimu wa kila kozi alafu muache mwenyewe achugue kozi akifuata amani yake hilo ndio KUSUDI lake. Ila mtoto anaweza akawa tayari wewe umchagulie na kukubaliana na wewe, hapo waweza kumchagulia kozi hiyo ya kusomea na kuweza baadae kums...

Umezaliwa kuleta mabadiliko chanya katika jamii inayo kuzunguka.

(Mathayo 13:33 Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke, akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia). Chachu yaani amila-wewe ni kama amila umeumbwa kuwachachua/kuwabadilisha watu wanaokuzunguka kutoka hali mbaya kwenda hali nzuri.Hakikisha Amila yako inafanya kazi ili kusaidia jamii. Hakikisha unafanya jambo lolote linaloweza kuisadia jamii iliyokuzunguka, tukisema jamii sio lazima uwaguse maelfu wote, anza kidogo kidogo na mtu, wawili n.k basi utaendelea kukua na kuzidi kuigusa zaidi jamii yako. Jiulize umefanya jambo gani zuri la kusaidia jamii iliyokuzunguka masaa 24 yaliyopita?

Wasikukatishe tamaa watu wanaoonekana kama wana mafanikio huku wakiwa na mwenendo mbaya.

Duniani tunaishi kama tunacheza movie/filamu.Binadamu wamepewa uhusika mbalimbali.Wengine wamepewa uhusika mbaya ili wawaimalishe wale wenye uhusika mzuri.Kwa hiyo mtu anaweza kuwa mbaya lakini akawezeshwa kuwa na uwezo wa mali na nguvu ili kumsukasuka mtu mwema na mtu huyu kujichunguza alipokosa na kumrudia Mungu, lakini yeye huyu mtu mbaya mwisho wake ni mbaya tu.Taifa la Israel kila lilipomkosea Mungu, Mungu aliwainua maadui zao na kuwaonea Israel, si kwamba adui wa Israel walifanya mema na kuinuliwa na Mungu, bali Mungu alitaka kuwarudisha Israel karibu na Mungu.Kweli walipotubu Mungu aliwarudia na kuwashinda adui zao. Sehemu nyingine mungu anasema usipotenda maagizo yake atakulaani na kukuletea taifa ambalo haliangalii makunyanzi na kukuonea na kula mali ya nchi yako na kukusukasuka mpaka uangamie.Hapa Taifa hili geni linainuliwa kuwa na nguvu na kukuonea si kwamba limetenda mema bali limewekwa katika uhusika mbaya chini ya jua. Vivyo hivyo kuna watu mmoja...

Rejea utafiti wako hapa.

1:Chukua makundi mawili ya vijana,kila kundi liwe na vijana kumi kumi.Vijana hawa anza kufuatilia maisha yao kwa miaka ishirini kuanzia wakiwa elimu ya sekondari. Kundi moja wawe wavuta bangi, sio watii,wagomvi,wapiganaji,waizi,watolo shuleni,wazinzi, wafiraji,wabakaji wenye matusi n.k. Kundi la pili wawe watulivu yaani wapole, watii,wanapenda shule,hawavuti bangi,si walevi,si wavuta bangi,si waizi na wapiganaji,si wazinzi,si wabakaji,si wafiraji n.k Je ni kundi gani linaweza kupatwa na mabaya kwa asilimia kubwa, na kundi lipi linaweza patwa na mema kwa asilimia kubwa? 2:Vivyo hivyo hata kwa watu wazima chukua familia mbili.Familia Moja walevi wanachelewa kurudi nyumbani,wazinzi,wala rushwa,wagomvi, visa na mapigano, hawaheshimu majirani,wakali, wanatukana majirani,wezi, waongo, wadhurumaji, wasengenyaji, wazushi, si watu wa haki, amani na upendo n.k Familia ya pili si walevi,wanawahi kurudi nyumbani na kukaa na watoto wao, si wazinzi,si wagomvi visa wala mapigano,wapole na...

Siri ya kula mema ya Nchi.

Ni maneno mawili KUKUBALI na KUTII .Unaweza ukawa mtii ila hujakubali,maana yake unatii ila lile uliloagizwa hujakubaliana nalo moyoni,hulipendi,unafanya kwa sheria tu, hapo bado inabidi uende mbele kidogo UTII na KUKUBALI ndipo utakapokula mema ya nchi. (Isaya 1:19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi) Tanatakiwa kukubaliana na kutii yale Mungu anayotuagiza,pia maagizo mema yoyote tunayoagizwa makazini kwetu,nchini kwetu inatakiwa kukubali na kutii. Hapo tutakula mema ya nchi.

Maisha ya Binadamu ni kama Mmea.

Jinsi kila mmea ulivyo na masharti,kama vile upandwe ktk aina gani ya udongo, kiwango cha mvua kinachohitajika   na muinuko mita ngapi.Vivyo hivyo Mwanadamu katika kila idara kama ndoa, malezi, uchumi Ulezi wa mimba n.k ana masharti.Unapokwenda kinyume na   Masharti huwezi pata matunda mazuri.Masharti haya yanatoka Kwenye neno la Mungu, neno la Mungu lina nguvu ndilo linaloshikilia Angani jua, nyota, mwezi, sayari zingine na ulimwengu mzima.Neno hilo hilo Limeshikilia idara mbali mbali katika maisha yako. (Zaburi 119 :105 Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.) Fuatilia Mungu anakuelekeza nini kwenye ndoa, malezi n.k Mfano -Katika malezi anasema mfundishe mtoto njia impasayo hata iacha atakapokuwa mtu mzima.Kwa hiyo ukiishia kumuombea tu mtoto bila kumfundisha ana asilimia kubwa sana ya kupotea. -Katika ndoa anasema enyi waume wapendeni wake zenu, na wake watiini waume zenu.maana yake usitegemee ustawi wa ndoa kama neno hili hal...

Ujumbe kwa wazazi na Vijana ambao ni wazazi watarajiwa.

(2 Wokorintho 12:14b maana haiwapasi watoto kuweka akiba kwa wazazi, bali wazazi kwa watoto).Hivyo wewe kijana mzazi tarajiwa au ndio umeanza kupata watoto tujipange kuweka akiba kwa watoto wetu tena tusiwe na mawazo ya kuja kuwategemea watoto wetu. Angalia pia hapo (Mithali 19:14a Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye). Pia (mithali 13:22 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi) Kumbe inatakiwa kwenda mbele zaidi, tuwe na mipango ya kuwezesha hata wajukuu zetu kurithi kitu kutoka kwetu. Upande wa Vijana msibweteke kusubiri urithi, neno linasema UTUKUFU wa mwisho utakuwa mkubwa kuliko ule wa kwanza.kama kijana inatakiwa hapo baadae kuja kuwa na mali zaidi ya walizokuwa nazo wazazi   wako, mfano kama ni nyumba/ basi   yako   iwe nzuri kuliko ya wazazi wako, sio kijana unaangalia kanyumba kamoja cha wazazi eti uje urithi.Ukiona kijana mpaka unaelekea utu uzima bado ni tegemezi kwa wazazi jua UNA MATATIZO maana na wewe sasa unaangaliw...

Usipigane na kila adui utachelewa kulea maono yako.

(Mathayo 2:13 Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize).Adui wengine wakimbie. Kumkimbia Adui si kimwili tu bali hata kimawazo.Unapomuwaza adui yako iwe kumuogopa au lolote la kumfanya, jua unapunguza/unadhoofisha maono yako ya vitu vya msingi.adui asitawale ktk mawazo yako kwani hiyo ni sehemu nyeti ya kupika maono yako.

Wewe ndiye mrithi wa Baraka.

Tambua wewe ni mrithi wa baraka kwa kazi iliyofanywa na wengine. Baraka zako ili uzichukue unatakiwa kufuata masharti haya. 1 petro 3:8-9 8 Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu; 9 watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.

Fumbua macho.

Mtu yoyote dunia lazima atakua mfanyakazi wa ufalme mmoja, shetani au Mungu.Na huwezi kusema mimi hapa dunia simtumikii yeyote, lazima unakua unatumika sehemu moja ila haujijui.Muda/Time unashikiliwa na kutumiwa na ulimwengu wa roho wa pande zote mbili tena kwa kuukomboa muda sana.basi ndani ya muda lazima utakuwa ndani ya ufalme mmoja.Jiulize Dakika tano ulizokaa ulikuwa unawaza nini, unafanya nini, unasoma nini, unaangalia nini, umevaa nini, unakunywa nini, una panga nini, unaongea nini, uko maeneo gani, unakusudia nini n.k kama yoote yanakubalika na Mungu jua hapo unatumikia ufalme wa Mungu. (Mathayo 6:24a Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu). Basi rafiki yang komboa muda bado hujachelewa.Kila wakati uwe mtu wa kujichunguza uko upande gani, kama uko upande mbaya basi unahama haraka.

Unapokunywa dawa - Usisahau hili.

Kama tulivyoona siri ya UZIMA/AFYA yako ni kulinda MOYO wako. (Mithali 4:23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima). Hii ndio Siri inayotuonyesha kwa upande wa kimwili kuwa dawa haziwezi kutibu magonjwa ya kufisha (yaletayo mauti), zinapunguza tu makali, au mtu atatakiwa anywe dawa maisha yake yote lakini bado ipo siku ugonjwa huo unalipuka na kumuondoa mgonjwa dunia. Ushauri:Mgonjwa anapoendelea kunywa dawa afanye ukarabati wa Moyo wake kwa kutubu dhambi na kuachia yote mabaya aliyoshikilia moyoni na kuendelea kuulinda moyo wake.Hivyo chemchem ya Uzima itaanza kububujika na kupambana na mauti iliyoingia kisha kupelekea uponyaji timilifu.Chemchem (Maji) ya Uzima yataanza kuflash maji ya mauti na kisha mauti kutokuwa na nguvu.

The Greatest Medicine for you.

(Proverbs 4:23 And keep watch over your heart with all care; so you will have life). Heart is a source of life. So you have to protect it as you protect source of water against contamination in order people to get clean water. When source of water is contaminated people will drink dirty water and get diseases. Your heart is created to carry light or good things in all of your life, that is a rule for human. Our hearts receive things through feelings. When you think things that cause you to feel bad you contaminate your heart and your life is affected. Some time your spouse, children, boss, enemy, friend etc can do something that can twist your mind and feel things that lead you to sadness or angry. According to Human Manual you are not allowed to feel in that direction. As we do diet of food to get good health also we have to do diet of our minds, do not dwell with every feelings. Below are things that our hearts have been created to think about; (Philippians 4:8 ...

Maisha/Uzima-Mambo yako yote yapo hapa.

(Mithali 4:23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima).Moyo wako ndio chanzo cha uzima/maisha/life.Kama ni maji ndio chanzo cha maji hakitakiwi kuchafuliwa.Hivyo moyo wako unatakiwa kuulinda kuliko chochote (fedha,magari n.k).Ukiruhusu mabaya katika moyo unakua umeharibu uzima wa kila kitu kama ndoa,afya,uzima wa roho n.k. Mabaya unayaruhusu vipi ndani ya moyo wako, ni kwa kuyatafakari/kuyawaza hapo unakua hujalinda moyo bali unakua umeingiza sumu kama kunywa maji ya betri.Moyo umeumbiwa kutafakari mambo mazuri tu, yenye sifa, tena yasiyokuumiza. Kwa kutafakari mambo mabaya yanayoleta chuki,hasira,kuhuzunika, kusononeka,kutosamehe,mambo yakupelekea kutenda dhambi-yamesababisha binadamu kupata magonjwa ya kimwili kabisa kwa sababu chazo cha uzima (Moyo) kimechafuliwa hivyo kimekuja kinyume cha uzima yaani mauti.Mfano wa kawaida hasira huleta maradhi ya pumu, kansa, kujiua n.k lakini pia unakosa uzima wa milele. (WAFILIPI 4:8 Hatimaye, ndug...

Siri ya kukuwezesha kutenda Matendo mema.

Ukisoma YOSHUA 1:8 Kuna sehemu anasema (yatafakari maneno yake mchana na usiku, UPATE kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo).Hiyo UPATE maana yake upokee/upewe uwezo wa kutenda.Kutafakari maneno ya Mungu ni kwa muhimu, unakuwa unayaingiza maneno moyoni.Siko zote mtu huongea maneno yaliyojaa moyoni, na hutenda anayoyaongea (kinywa kina nguvu), na anayoyatenda ndio huleta miisho mizuri au mibaya.YOUR THOUGHTS CONTROL YOUR WORDS, YOUR WORDS CONTROL YOUR ACTION, AND YOUR ACTION DETERMINE YOUR DESTINY. NYONGEZA:Somo linatuonyesha ukitafakari/kuwaza mabaya, utatenda mabaya na miisho yako itakua mibaya.Ukitafakari mazuri tegemea mazuri. Unachotafakari ni mbegu,unatafakari nini sasa?

Siri ya Mungu kutembea na wewe.

WAFILIPI 4:8-9 8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo. 9 Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi. (Ukitafakali mambo yote mabaya kama chuki,tamaa,dhuruma,wizi,masengenyo n.k hapo Mungu anakuwa hayupo nawe unakuwa unafanya kazi katika ulimwengu wa shetani nguvu za giza.Muda hutumiwa na ulimwengu wa roho tena kwa kuukomboa, sasa katika muda wako lazima uwe upande mmoja wa ulimwengu wa shetani au Mungu.Kujijua uko upande gani kipimo ni unatafakari nini, kama hutafakari mambo mazuri kama yaliyotajwa hapo juu, ujue upo unafanya kazi katika ulimwengu wa shetani).Sasa rafiki ni wakati wa kuukomboa muda, kwa kutafakari mambo mema ya Mungu, hapo atakuwa nawe, akiwa nawe yeye ni kila kitu,uponyo uta...

Njia ya kwenda kuchukua mafanikio.

Kumbukumbu la torati 28:1-8 1 Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; 2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako. 3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. 4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. 5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. 6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo. 7 BWANA atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. 8 BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.

Kama watoto wa Mungu inatakiwa tumfuate Mungu.

Kama watoto wa MUNGU inatakiwa kufuata tabia za Mungu kama uzao wake.mfano mtoto wa mnyama yoyote hufuata tabia zao.na sisi kama watoto wa Mungu, tunafuata tabia za Mungu.Mungu ni upendo anawapenda wabaya na wema hivyo nasi tunatakiwa kuwapenda adui zetu, kuwaombea wanaotuuzi na kuwabariki wanaotulaani. Kama hufanyi hivyo wewe unakuwa sio mwana wa Mungu.kama sio mwana wa Mungu utakua mwana wa nani?Chukua hatua za kubadilika haraka. Wafeso 5:1 (Ephesians 5:1) 1 Hivyo mfuateni Mungu, kama watoto wanaopendwa; 1 Therefore, be imitators of God as dearly loved children.

Jipime - Mtoto wa Mungu ana tabia hizi.

-Anawapenda maadui zake. -Anawabariki wanao mlaani. -Anakuwa na huruma. Endelea chini Luka 6:27-38 27 Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi, 28 wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi. 29 Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang’anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu. 30 Mpe kila akuombaye, na akunyang’anyaye vitu vyako, usitake akurudishie. 31 Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo. 32 Maana mkiwapenda wale wawapendao ninyi, mwaonyesha fadhili gani? Kwa kuwa hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao. 33 Nanyi mkiwatendea mema wale wawatendeao mema, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo. 34 Na mkiwakopesha watu huku mkitumaini kupata kitu kwao, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, ili warudishiwe vile vile. 35 Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema,...

Kutenda wema hakuna hasara

Mtu mmoja alituhadithia, jana wakati wao wadogo, walipomtembelea mama yao mdoko, aliwatengea chakula pamoja na watoto wa mama yake mdogo. wakati wanaendelea kula mama yake mdogo alimkata jicho hilo (alimtaza vibaya) kiasi kwamba jamaa alishusha tonge chini, alafu mama huyo akawatazama watoto wake kwa jicho la nyie zubaeni   tu ili waongeza speed, lakini akimtaza yeye ni kwa jicho la kumpunguza speed kula.Jamaa anasema watoto wa huyo mama walikua sita ila kwa sasa wa kwanza alikufa, wa pili ametolokea nchi   za watu hajulikana aliko mpaka leo, watatu teja yupo nyumbani wa nne na wa tano hawaeleweki shule zimewashinda wapo nyumbani na wa mwisho ni mdogo. mama huyo hana msaada. Tunajifuza unapokuwa mchoyo unajilaani wewe na uzao wako. Unaweza ukawa mchoyo wa mawazo mazuri au mbinu mbalimbali za maisha kwa jamii inayo kuzunguka. Wape watu mawazo mazuri ili wafanikiwe, usiwape tu wale wa karibu unaowajua na kuwapenda. Jina la mtu halikumbukwi kwa sabab...