Skip to main content

Wasikukatishe tamaa watu wanaoonekana kama wana mafanikio huku wakiwa na mwenendo mbaya.

Duniani tunaishi kama tunacheza movie/filamu.Binadamu wamepewa uhusika mbalimbali.Wengine wamepewa uhusika mbaya ili wawaimalishe wale wenye uhusika mzuri.Kwa hiyo mtu anaweza kuwa mbaya lakini akawezeshwa kuwa na uwezo wa mali na nguvu ili kumsukasuka mtu mwema na mtu huyu kujichunguza alipokosa na kumrudia Mungu, lakini yeye huyu mtu mbaya mwisho wake ni mbaya tu.Taifa la Israel kila lilipomkosea Mungu, Mungu aliwainua maadui zao na kuwaonea Israel, si kwamba adui wa Israel walifanya mema na kuinuliwa na Mungu, bali Mungu alitaka kuwarudisha Israel karibu na Mungu.Kweli walipotubu Mungu aliwarudia na kuwashinda adui zao.
Sehemu nyingine mungu anasema usipotenda maagizo yake atakulaani na kukuletea taifa ambalo haliangalii makunyanzi na kukuonea na kula mali ya nchi yako na kukusukasuka mpaka uangamie.Hapa Taifa hili geni linainuliwa kuwa na nguvu na kukuonea si kwamba limetenda mema bali limewekwa katika uhusika mbaya chini ya jua.
Vivyo hivyo kuna watu mmoja mmoja ambao wanakua wamefanikiwa alafu wanatenda mambo mabaya hao wanakua wamewekwa katika uhusika wa watu wabaya chini ya jua , wengine wanaoneka dhahiri wakitumia mali zao kuwaonea watu, watu hawa usiwaige wamewekwa katika uhusika mbaya chini ya jua na miisho yao ni mibaya.

Pia shetani ana watu wake ambao huwapa mali ili kuimarisha utawala wa shetani duniani.Watu wa jinsi hii hufanikiwa lakini uhusika wao ni mbaya kwani hutumia mali walizo nazo kufanya matendo maovu/dhambi yanayoimarisha ufalme wa kishetani duniani.Shetani ana mali tena kimaandiko ni mungu wa dunia.Alimwonyesha Yesu Milki/Mali zake akamwambia ukinisujudia nitakupa milki hizi,Yesu alijua kisheria zilikua za shetani kwani alimdanganya mwanadamu wa kwanza akachukua milki yote aliyokabidhiwa, basi Yesu akamjibu imeandikwa msujudie Bwana Mungu wako na si mwingine.Shetani akamuacha malaika wakaja kumtumikia.Wewe umepataje kazi,mali,tenda kwa kumsujudia shetani kupitia kutoa au kupokea rushwa? Sasa shetani hawezi kuondaka na malaika hawawezi kukutumikia.Kama ulifanya hivyo ulikuwa hujui, tubu kwa Mungu alafu usirudie tena.


Angalia neno hili chini linavyoonyesha jinsi mtu mbaya anavyoweza inuliwa kutumiwa kama fimbo ya laana pale mtu wa Mungu anapokosea.

Kumbukumbu la torati 28:15,49,50,51,52
-15 Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.
-49 BWANA atakuletea taifa juu yako kutoka mbali, kutoka ncha ya dunia, kama arukavyo tai; taifa usiloufahamu ulimi wake;
-50 taifa lenye uso mkali, ambalo haliangalii uso wa mzee, wala halipendelei kijana;
-51 naye atakula uzao wa ng’ombe wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako mpaka utakapokwisha kuangamizwa; wala hatakuachia nafaka, wala divai, wala mafuta, wala maongeo ya ng’ombe wako, wala wana-kondoo wako, hata atakapokwisha kukuangamiza.
-52 Naye atakuhusuru katika malango yako yote, hata kuta zako ndefu, zenye maboma, ulizokuwa ukiziamini, zishuke, katika nchi yako yote kila upande; naye atakuhusuru katika malango yako yote kila upande, katika nchi yako yote aliyokupa BWANA, Mungu wako.

Basi usiyumbishwe ndugu yangu.Vumilia endelea kufanya mambo mazuri ya kumpendaza usizimie moyo, Mungu atakubarki kwa wakati wake.Endelea kujifunza na kuongeza maarifa, huenda kuna sehemu ndogo sana unakosea.Mungu anasema watu wangu wabaangamia kwa kukosa maarifa.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA LUKUKI UNAZOPATA UNAPOOMBA KILA SIKU. (WHY DAILY PRAYER IS IMPORTANT)

Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa-Luka 18:1. i-Unapoomba, ahadi za Mungu alizoziahidi kwako zinatimia. Mungu aliahidi atatutupa Roho mtakatifu, lakini Roho mtakatifu alishuka kwa mitume wakiwa katika kuomba siku kumi. Sehemu nyingine Mungu anasema huwapa thawabu wale wamtafutao. Unapoomba upo katika kitendo cha kumtafuta Mungu, kwa hiyo kuna vitu vingine vizuri huwa anakupa ukiwa unaomba hata kama hujaviomba. Kwa hiyo kama huombi hupati ahadi zako.Kwani shetani anakua na nguvu ya kuzivuruga na kuleta vikwazo. Waebrania 11: 6 – “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”.   ii-Unapoomba ni sawa na binadamu anavyohema kwa kuvuta hewa safi (oxygen) na kutoa nje hewa chafu (cabon), ukiomba unavuta paradiso ndani yako na kutoa nje heeee Dunia, au unamvuta Yesu ndani na kutuoa nje heee ubinadamu.Sasa unapoomba kila siku Yesu

SHARTI LILILOJIFICHA KWA AJILI YA UPONYAJI WA MWILI WAKO.

  Mungu anataka kukuponya lakini ili akuponye shariti lake ni hili; (Warumi 8: 11…Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu)   Unaona sharti hilo- ameanza na neno “Lakini, ikiwa” maana yake hilo ni sharti yaani ukiwa na Roho aliyemfufua Kristo Yesu yaani Roho wa Mungu au Roho mtakatifu ndani yako ndio utapata uponyaji kamili. Lakini kinyume chake hakuna uponyaji.   Sasa kumbe unahitaji kujua utampataje huyo Roho Mtakatifu na kumtunza kwa faida ya Roho na Mwili wako. Maana yake kama hauna huyo uko hatarini. (i)Tubu dhambi zako zote kwa Mungu-Maana Roho mtakatifu anataka awe yeye mwenyewe tu ndani yako. Moyo wako uwe kama karatasi nyeupe isiyokuwa na doa. (ii)Anza kuishi maisha ya kitakatifu kama kutokua na na chuki, kujiinua, hasira, woga, hofu, dharau, kuwaza mambo mabaya yaliyopita au uliyoten

KITU KINACHOMUATHIRI BINADAMU KUTOFIKIA MALENGO YAKE.

Nyumba hujengwa kwa hekima (methali 24:3a) Hapa tunajifunza chocote kinachojengwa ili kifanikiwe kinahitaji Hekima, Bila Hekima chochote hakiwezi jengeka vizuri bali kitakuwa kinaharibiwa. Hapa nakuonyesha vitu vichache ambavyo unavijenga ili vifanikiwe vinahitaji Hekima; -Unajenga ndoa (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga watoto wako wawe wacha Mungu, pia wawe watu wazima wajitegemee na wawe msaada katika taifa (Inahitaji Hekima bila hiyo wanaharibika) -Unajenga kampuni, taasisi, biashara, kikundi, kazi, nchi (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga ujirani mwema (Inahitaji Hekima bila hiyo unaharibika) -Unajenga afya yako(Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Kumjenga au kumfundisha mtu kunataka hekima-bila hivyo utamvuruga kabisa. Hiyo ni mifano ya vitu vichache-lakini kumbuka chochote unachofanya unajenga na kinahitaji hekima. Hekima ni muhimu sana katika maisha yetu, mfalme Sulemani alipoambiwa na Mungu omba chochote aliomba Hekima.