Faida za kulea watoto mliowazaa na msio wazaa, wajomba, mashangazi, wajukuu, wadogo zenu, wazazi wenu,baba na mama wadogo, bibi babu n.k
WAKOLOSAI 3:23-24
23 Lo lote mfanyalo,
lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu,
24 mkijua ya kuwa
mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo.
Nakushauri walee watu
hao kwa moyo wako wote kama unamfanyia mungu na si unamfanyia mwingine
aliyepaswa kulea, kwani kuna baraka nyingi sana.wewe jaribu kuwalea kwa moyo
wote utaanza kuona baraka endelevu zikimwagika juu yako, jinsi unavyo kaa nao
nawe ndio jinsi mvua ya baraka inavyoendelea kukunyeshea.wape mahitaji
wanayostahili kama; vitanda vizuri, mablanket mazuri na mazito, chakula cha
kutosha, nguo, viatu n.k wewe jiachie kwao kwani ukiwalea kwa shingo upande
huwezi kupata thawabu, miaka yooote ulio kaa nao itakua bure, itakua hasara.
Kumbuka wahitaji hao
wanaweza kukutendea mabaya, kama kukusengenya, manung’uniko, kutokukutii vyema,
kukuibia n.k wewe usiangalia hayo, samehe na endelea kuwahudumia ipasavyo.
aloooo kwa kufanya
vyema hivyo tegemea baraka za hali ya juu.
Comments
Post a Comment