Methali 15:4 “Ulimi safi ni mti wa uzima; Bali ukorofi wa
ulimi huvunja moyo”.
Maana yake ulimi wako ukiongea huku ukiwa na asili ya faraja
basi unayeongea nae utampa uzima yaani kubadilika kutoka njia mbaya kwenda njia
nzuri.
Biblia ya kiingereza ulimi safi inaita comforting
tongue/yaani ulimi wa kutia moyo/kufariji.
Zingatia katika lolote unalomwambia mtu ulimi wako uwe na
munyu huu wa faraja/comforting, aah utaponya wengi.Kinyume chake utawavunja
moyo wengi na kuua wengi.Unapoongea,kufundisha HAKIKISHA unaongea huku ukiwa na
UPENDO, kwa kufanya hivyo utajikuta maongezi, mafundisho yako yanayotoka
ulimini mwako yanakua na faraja/kutia moyo na kupelekea mtu kupata uzima katika
eneo lililokufa au linalotaka kufa.
Tumia njia hii;
-unapofudisha mtoto wako.
-katika mazungumzo,maeleweshano mume na mke.
-mchungaji ukihubiri kama hutumii njia hii utashangaa
waumini wanakufa, wanakufa hata kama ni neno la Mungu.Mafundisho yako usimpanie
mtu, fundisha kwa upendo.
-tumia comforting tongue katika biashara.
-tumia comforting tongue sehemu unapotaka kutokea ugomvi.n.k
-unapoongea na wafanya kazi wako.
Neno linasema (mambo yote yafanyike kwa upendo/Let Love
lead, Let love be the UPPERMOST in your life). Mambo yakifanyika kwa upendo
yanakuwa hai, kwani mambo yote yanapita ila UPENDO unasalia.
(A comforting tongue is a tree of life, but a twisted tongue
is a crushing of the spirit)
Comments
Post a Comment