KUWA NA SIKU NJEMA
1 PETRO 3:10-11 Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona
siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila.
11 Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate
sana.
-Hii ni kanuni ya kufanya malengo yako ya siku
yafanikiwe.Bila kufuata kanuni hiyo maana siku hiyo haitakua njema bali mbaya
kama kupoteza vitu, kuibiwa,kuumia,kuugua,kufukuzwa
kazi,kupigana,kugombana,kutouza bidhaa, kutokua na amani,kupigwa na
kichaa,kuangukiwa na mti/ukuta, yaani kuwa na nuksi kwa ujumla.Kwa kufuata
kanuni hizo za mistari hii miwili, utapenda maisha/utaenjoy maisha (ndio maana
anasema atakaye kupenda maisha .....) kwa hiyo mtu ambaye hufuati kanuni hii
hufurahii maisha, badilika sasa ili zije nyakati za burudani.
Maisha yako chini yako.
Neno hili linatuangazia kuwa kuifanya siku kuwa njema/maisha
mema kupo chini ya uwezo wako.
Tumeona moja ya siri
ya kuwa na siku/maisha mema ni kuzuia ulimi usinene mabaya.Ulimi kunena
mabaya ni kutukana, kujibu vibaya, kusengenya,kulaani.Lingine lililo jificha ni
kujinenea vibaya kusema mimi mjinga, msahaulifu, mgonjwa, maskini, siwezi.kwa
hiyo anataka ulimi wako unene mema, yaani bariki wengine,jitamkie mema mwenyewe
sema mimi ni TAJIRI,NURU,NINA AFYA NJEMA,MTOTO WA MFALME, MTATUZI WA MATATIZO
DUNIANI/PROBLEM SOLVER & SOLUTION BRINGER.n.k
Comments
Post a Comment