Binadamu hufananishwa na mti wa matunda.
Hivyo binadamu anatakiwa azae matunda mazuri.
Matunda ni kitu ambacho huchumwa na kumnufaisha mchumaji.
Matunda yanayozungumziwa hapa ni tabia njema/matendo ya
kumpendeza Mungu na pia matendo ya kuwapendeza wanadamu na kunufaika kutokana
na wewe.Jiulize tabia zako ni njema kwa Mungu na watu wanaokuzunguka, watu
wanasemaje kuhusu wewe.Jina lako likitajwa mbele za watu huona matunda gani
kwako/au picha gani ya haraka hutokea kwao (mfano mwizi, Malaya, tapeli, mkali,
muongo, mgomvi, msengenyaji, mchafu, mlevi/cha pombe, mzushi, mpole, mwaminifu,
mchapaka kazi, mtenda haki, ana upendo n.k).
Pia jiulize watu wanaokuzunguka (jirani zako, serikali yako
ya mtaa, familia na ndungu zako n.k) wanafaidika na nini kutoka kwako maana
tunda lazima pia limfaidishe mtu wa upande wa pili.
Au wewe ndio umekua chanzo cha migogoro na kutia hasara
katika familia, kazi, ukoo, mtaa, vikundi n.k. Basi Rafiki yangu kama uko kundi
baya badilika maana uko hatarini sana, nje ya hatari, yaani wewe unakuwa kitu
kibaya duniani (kama unavyoona mimea mingine mibaya na na wadudu wabaya) Yaani
wewe unakuwa“mti unaozaa matunda Pori/sumu au unakuwa KIRUSI/VIRUS.
Usikubali kuwa kitu kibaya Duniani.
Mathayo 3:10
10 Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi
kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.
BE FRUITFUL
Comments
Post a Comment