(2 Wokorintho 12:14b maana haiwapasi watoto kuweka akiba kwa
wazazi, bali wazazi kwa watoto).Hivyo wewe kijana mzazi tarajiwa au ndio
umeanza kupata watoto tujipange kuweka akiba kwa watoto wetu tena tusiwe na
mawazo ya kuja kuwategemea watoto wetu.
Angalia pia hapo (Mithali 19:14a Nyumba na mali ni urithi
apatao mtu kwa babaye).
Pia (mithali 13:22 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe
urithi) Kumbe inatakiwa kwenda mbele zaidi, tuwe na mipango ya kuwezesha hata
wajukuu zetu kurithi kitu kutoka kwetu.
Upande wa Vijana msibweteke kusubiri urithi, neno linasema
UTUKUFU wa mwisho utakuwa mkubwa kuliko ule wa kwanza.kama kijana inatakiwa
hapo baadae kuja kuwa na mali zaidi ya walizokuwa nazo wazazi wako, mfano kama ni nyumba/ basi yako
iwe nzuri kuliko ya wazazi wako, sio kijana unaangalia kanyumba kamoja
cha wazazi eti uje urithi.Ukiona kijana mpaka unaelekea utu uzima bado ni
tegemezi kwa wazazi jua UNA MATATIZO maana na wewe sasa unaangaliwa uwekeze
uwaachie urithi watoto wako na wajukuu zako.(Hagai 2:9a Utukufu wa mwisho wa
nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema BWANA wa majeshi).
Comments
Post a Comment