Skip to main content

IN THE NAME OF JESUS I PUNCH MY ENEMY WITH UPPERCUT.

IN THE NAME OF JESUS I PUNCH MY ENEMY WITH UPPERCUT (Nilikua mcheza Ngumi/Bondia- uppercut ni ngumi mbaya unamchimba adui akiinama kutoka chini kuja juu.sasa huyu anaomba anampiga adui hii ngumi).IN THE NAME OF JESUS I PUT MY ENENEMY IN THE COFFIN(anaomba anamuweka adui yake ndani ya jeneza maana yake afe ) SISI MAOMBI YETU SIO YA KUUA, BALI TUNAOMBEA MABAYA ALIYOKUSUDIA ADUI YASITUPATE.USIOMBE HIVI-MFANO UNAOMBA UNASEMA "BWANA NAKUSIHI ADUI FULANI USIMWACHE, UNAKUMBUSHA UNASEMA BWANA UMESEMA WEWE NDIYE ULIPAYE KISASI TENDA BWANA, TENDA BWANA(yaani ampige adui yako)
USIFANYE HIVYO KABISA HAUTAKUWA MTOTO WA MUNGU. KANUNI MOJA YA KUWA MTOTO MUNGU NI KUWAPENDA ADUI KAMA NENO LINAVYOSEMA.KWA HIYO UKIMPENDA ADUI HUWEZI KUMUOMBEA MABAYA AU KUKUMBUSHIA HASIRA YA MUNGU JUU YA ADUI.UKIONA MAOMBI YAKO NI YAKUMKUMBUSHA MUNGU KUMPIGA ADUI UJUE UPENDO HAUPO NDANI YAKO, NA KAMA HUNA UPENDO UJUE HUNA MUNGU.MUNGU NI UPENDO, KAMA HAMNA UPENDO HAMNA MUNGU. STEFANO ALIPIGWA NA MAWE KIMWILI NA KUSIKIA HARUFU YA MAUTI LAKINI ANAOMBA MUNGU USIWAHESABIA DHAMBI WANAOMPIGA HADI WALIMWUA .NAWAZA UKIFIKIA KUTESWA KAMA STEFANO UTAOMBAJE JUU YA WATESI WAKO, KAMA TU KATIKA VIMATESO HIVI VIDOGO UNAMWAMBIA MUNGU ASIWAACHE MAADUI ZANGU NA KUKUMBUSHIA HASIRA ZAKE JUU YA MAADUI ZAKO TENA KWA KILIO. UNAPOITA MUNGU AWAPIGE MAADUI ZAKO MAANA YAKE MUNGU ASISAMEHE.
SASA SIKILIZA MTOTO WA MUNGU HALISI ANAKUWA NA DNA/VINASABA VYA BABA YAKE MUNGU KAMA UPENDO,KUSAMEHE, UVUMILIVU N.K. MTOTO WA MUNGU SIKU ZOTE NI MPATANISHI, ANAWAPATANISHA WAOVU NA BABA YAKE.NDIO MAANA NENO LINASEMA Heri wapatanishi maana hao wataitwa WANA wa MUNGU.KAMA UNAKUMBUSHIA MUNGU KUPIGA MAADUI, UNAKUA SIO MPATANISHI/YAANI SIO MWANA WAKE.
PAULO UNAYEMSIKIA KABLA HAJAOKOKA ALISHIRIKI KUMUUA STEFANO, LAKINI KWA MAOMBI MEMA STEFANO YA ALIYOWAOMBEA KWA MUNGU, PAULO ALIOKOLEWA.BAADA YA KUMUUA STEFANO PAULO ANAKWENDA DAMESKI NA FARASI KUWATESA WATU WA MUNGU WENGINE, MUNGU ANAMTOKEA KWENYE FARASI PAULO KIPINDI HICHO ANAITWA SAULI ANAANGUKA, ANAMWAMBIA SAULI MBONA WANIUDHI? PAULO ANAOKOLEWA NA MUNGU NA AKAWA MTUME WA MUNGU MWENYE NGUVU SANA ALIYEWALETA WATU WENGI KWA MUNGU NA TUNAMSOMA HADI LEO, YOTE HAYO NI MAOMBI YALIYOPANDWA NA STEFANO.SASA NA WEWE TUMIA NGUVU KUBWA KUWAOMBEA ADUI ZAKO MUNGU AWASAMEHE NA AWAOKOE HAPO UTAKUWA MPATANISHI/MWANA WA MUNGU. JIFUNZE KWA MTOTO WA MUNGU YESU, ALIVYOFANYA KWA MAADUI ZAKE; ALISAMEHE WALIPOKUA WANAMUUA ALISEMA WASAMEHE HAWAJUI WALITENDALO-WEWE UMEFIKIA KUTESWA SAWA NA YESU HATA USITAMKE NENO WASAMEHE' WEWE NI KUOMBA KUTANAO BABA, TENDA BWANA yaani awapige.SEHEMU NYINGINE MWANAFUNZI ALIKATA MTU SIKIO KATI YA WALE WALIOKUJA KUMSHURUTISHA YESU, LAKINI YESU AKARUDISHIA.
Nikupe siri-ukiona maombi yako au moyo unatamani maadui kupigwa jua aidha ni mwanafunzi/yaani mchanga/mtoto sana/ tunaelewa mtoto hawezi kuwa mrithi wa ufalme mpaka akue.Mbili aidha una roho mbaya inakumiliki na imekomaa, yaani unakuwa ni adui aliyejiingiza kwa siri(unaona hatari hii?)
Kipindi hiki tupo kwenye AGONO JIPYA NA MUNGU, Naweza sema MKATABA MPYA.kwenye Agano jipya hakuna tunaporuhusiwa kumuombea mtu mabaya.AGANO LA KALE waliruhusiwa kulipa baya kwa baya lakini sio sasa.Sasa tupo AGANO JIPYA (Tafakari neno AGANO JIPYA maana yake kuna upungufu kwa lile la zamani (AGANO LA KALE)
Waebrania 8:7&13
7 Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili.
13 Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka.

Unaona! Kwasasa MUNGU anataka tufanye hivi, ili tuwe watoto wake na kufikia kiwango cha utakatifu anachokitaka,soma hapo chini;

Mathayo 5: 44-48
44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?
48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Asante.


Comments

Popular posts from this blog

FAIDA LUKUKI UNAZOPATA UNAPOOMBA KILA SIKU. (WHY DAILY PRAYER IS IMPORTANT)

Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa-Luka 18:1. i-Unapoomba, ahadi za Mungu alizoziahidi kwako zinatimia. Mungu aliahidi atatutupa Roho mtakatifu, lakini Roho mtakatifu alishuka kwa mitume wakiwa katika kuomba siku kumi. Sehemu nyingine Mungu anasema huwapa thawabu wale wamtafutao. Unapoomba upo katika kitendo cha kumtafuta Mungu, kwa hiyo kuna vitu vingine vizuri huwa anakupa ukiwa unaomba hata kama hujaviomba. Kwa hiyo kama huombi hupati ahadi zako.Kwani shetani anakua na nguvu ya kuzivuruga na kuleta vikwazo. Waebrania 11: 6 – “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”.   ii-Unapoomba ni sawa na binadamu anavyohema kwa kuvuta hewa safi (oxygen) na kutoa nje hewa chafu (cabon), ukiomba unavuta paradiso ndani yako na kutoa nje heeee Dunia, au unamvuta Yesu ndani na kutuoa nje heee ubinadamu.Sasa unapoomba kila siku Yesu

SHARTI LILILOJIFICHA KWA AJILI YA UPONYAJI WA MWILI WAKO.

  Mungu anataka kukuponya lakini ili akuponye shariti lake ni hili; (Warumi 8: 11…Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu)   Unaona sharti hilo- ameanza na neno “Lakini, ikiwa” maana yake hilo ni sharti yaani ukiwa na Roho aliyemfufua Kristo Yesu yaani Roho wa Mungu au Roho mtakatifu ndani yako ndio utapata uponyaji kamili. Lakini kinyume chake hakuna uponyaji.   Sasa kumbe unahitaji kujua utampataje huyo Roho Mtakatifu na kumtunza kwa faida ya Roho na Mwili wako. Maana yake kama hauna huyo uko hatarini. (i)Tubu dhambi zako zote kwa Mungu-Maana Roho mtakatifu anataka awe yeye mwenyewe tu ndani yako. Moyo wako uwe kama karatasi nyeupe isiyokuwa na doa. (ii)Anza kuishi maisha ya kitakatifu kama kutokua na na chuki, kujiinua, hasira, woga, hofu, dharau, kuwaza mambo mabaya yaliyopita au uliyoten

KITU KINACHOMUATHIRI BINADAMU KUTOFIKIA MALENGO YAKE.

Nyumba hujengwa kwa hekima (methali 24:3a) Hapa tunajifunza chocote kinachojengwa ili kifanikiwe kinahitaji Hekima, Bila Hekima chochote hakiwezi jengeka vizuri bali kitakuwa kinaharibiwa. Hapa nakuonyesha vitu vichache ambavyo unavijenga ili vifanikiwe vinahitaji Hekima; -Unajenga ndoa (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga watoto wako wawe wacha Mungu, pia wawe watu wazima wajitegemee na wawe msaada katika taifa (Inahitaji Hekima bila hiyo wanaharibika) -Unajenga kampuni, taasisi, biashara, kikundi, kazi, nchi (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga ujirani mwema (Inahitaji Hekima bila hiyo unaharibika) -Unajenga afya yako(Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Kumjenga au kumfundisha mtu kunataka hekima-bila hivyo utamvuruga kabisa. Hiyo ni mifano ya vitu vichache-lakini kumbuka chochote unachofanya unajenga na kinahitaji hekima. Hekima ni muhimu sana katika maisha yetu, mfalme Sulemani alipoambiwa na Mungu omba chochote aliomba Hekima.