1:Chukua makundi mawili ya vijana,kila kundi liwe na vijana
kumi kumi.Vijana hawa anza kufuatilia maisha yao kwa miaka ishirini kuanzia
wakiwa elimu ya sekondari.
Kundi moja wawe wavuta bangi, sio
watii,wagomvi,wapiganaji,waizi,watolo shuleni,wazinzi, wafiraji,wabakaji wenye
matusi n.k.
Kundi la pili wawe watulivu yaani wapole, watii,wanapenda
shule,hawavuti bangi,si walevi,si wavuta bangi,si waizi na wapiganaji,si
wazinzi,si wabakaji,si wafiraji n.k
Je ni kundi gani linaweza kupatwa na mabaya kwa asilimia
kubwa, na kundi lipi linaweza patwa na mema kwa asilimia kubwa?
2:Vivyo hivyo hata kwa watu wazima chukua familia
mbili.Familia Moja walevi wanachelewa kurudi nyumbani,wazinzi,wala
rushwa,wagomvi, visa na mapigano, hawaheshimu majirani,wakali, wanatukana
majirani,wezi, waongo, wadhurumaji, wasengenyaji, wazushi, si watu wa haki,
amani na upendo n.k
Familia ya pili si walevi,wanawahi kurudi nyumbani na kukaa
na watoto wao, si wazinzi,si wagomvi visa wala mapigano,wapole na wanaheshimu
majirani,si watukanaji, si waongo, si wadhurumaji, si wazushi, watu wa
haki,amani na upendo n.k
Fuatilia familia hizi kwa miaka kumi, Familia ipi inaweza
kupatwa na mabaya kwa asilimia kubwa, na familia ipi inaweza pata mema kwa
asilimia kubwa?
Hilo ndio jibu la
(Isaya 1:19 Kama MKIKUBALI na KUTII mtakula mema ya nchi)
Comments
Post a Comment