Binadamu aliyefanikiwa ni mtu ambaye ni msaada katika jamii
iliyomzunguka.
Mtu wa namna hii anafananishwa na Mti unaozaa matunda.
Katika jamii zetu kuna makundi mbali mbali yanahitaji
msaada, sehemu nyingine sio fedha ni mawazo tu na kuwatia moyo.
Hatari ni hii-kama wewe ni mtu mzuri wa maadili, unajilinda
sana/msafi sana, hutendi dhambi, ila unajiishia mwenyewe na familia yako,
husaidii watu wenye shida unafananishwa na mti ambao upo lakini hauzai matunda.
Hatari ni kwamba unaonekana ni mti ambao unabana nafasi na pia unaharibu ardhi.
(LUKA 13:7 Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu,
Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate
kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu?)
Binadamu ni mfanao wa miti ya aina tatu.
-Mti wa kwanza ni ule unaozaa matunda mazuri (yaani huyu ni
yule mtu ambaye hatendi dhambi ni msafi na anasaidia jamii iliyomzunguka, watu
wanafaidika kutoka kwake. Huyu ana Heri)
-Mti wa pili ni ule
unaozaa matunda mabaya (Mtu huyu huwafanyia watu wengine mambo mabaya ya
kuwaumiza kama kuwatukana, kuwaibia, kuwasenginya, kuwaua n.k. watu hawafaidiki
na lolote kutoka kwake bali ni maumivu tu, Mtu huyu ni mtenda dhambi. Mtu wa
jinsi hii Ole imesimama kwake)
-Mti wa tatu upo unaonekana lakini hauzai matunda (yaani
huyu ni mtu anajilinda na dhambi lakini hajishughulishi kwa ajili ya wengine,
anahesabika hazai matunda. Mtu wa jinsi hii yuko hatarini asipobadadilka na
kuanza kuwatendea wengine mema,kuzaa matunda kama neno linavyosema hapo juu
LUKA 13:7)
Yesu atakapokuja kuhukumu ataangalia matendo mema uliyowatendea
wengine
Mathayo 25:34-45
34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume,
Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu
kuumbwa ulimwengu;
35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na
kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;
36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja
kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.
37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini
tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?
38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u
uchi, tukakuvika?
39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni,
tukakujia?
40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri
mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto,
Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari
Ibilisi na malaika zake;
42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na
kiu, msininyweshe;
43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike;
nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.
44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini
tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au
u kifungoni, tusikuhudumie?
45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri
msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
Sasa ni muda wako wa kuzaa matunda.
Mfano kuna vijana katika eneo lako wapo vijiweni-Sasa
ilitakiwa wewe mwenye maadili, msomi na mwenye uwezo kuwatembelea vijana hao
siku moja moja, sio kukaa peke yako na kuishia kuwasema tu (wavuta bangi wale,
waizi wale). Inatakiwa kutoka na kuongea nao kwa upendo kuwaelekeza wanatakiwa
kufanya nini waweze kusonga mbele. Kwa kufanya hivyo unatawatia nguvu na
kuwaonyesha maisha mengine mazuri.Vijana wengi wanaingia vijiweni na kukosa
makaka wazuri wakuwaelekeza maisha, sasa tunawaachia makaka wabaya wanawapokea
na wanawaelekeza kuvuta bangi na kuiba.Tunawaachia makaka wabaya wanawaonyesha
maisha mabaya na vijana kuona HAYA NDIO MAISHA ya kuvuta bangi, kuiba, kwenda
jela na kutoka.
Wewe kwa kwenda wanapokuona tu, kuna kitu unawavuvia
wanaanza kutamani maisha yako yanayo kubalika, wanatamani kuwa kama wewe.
Unaweza ukawa kwa upande wako huwezi kuanza kuwaingia,
watafutie watu wenye uwezo huo, watafutie program/programme/project za
kuwasogeza mbele, fanya wewe kuwa kiunganishi kati yao na fursa mbalimbali
unazoweza kuziona na kuwaunganisha. Sehemu nyingine huenda unakumbana na fursa
zao ila hufanyi connection/uunganishi wowote unaziacha zinawapita.
Pia kuna wasichana katika eneo lako wanahitaji msaada wa mawazo
mazuri hata fedha kwa ajili ya mitaji midogo midogo, ni kazi yako wewe dada/
kaka/baba/mama kuwasaidia. Usiwaachie watu wabaya kuwaelekeza vijana wetu maisha
mabaya. Sasa ni muda wewe kuwa URGENT OF CHANGE katika jamii yako.
Onyesha thamani yako kwa kufanya mabadiliko katika jamii
yako.Usiishie kwenda kazini na baaada ya kurudi nyumbani na kujifungia ndani.
Anza kidodogo kwani Mungu anapenda tujishughulishe kwa ajili
ya wengine.
Mungu amekubariki na kukufundisha maadili yake si kwa ajili
yako peke yako kwani atakudai. Tumia chochote alichokupa Mungu kiwafaidishe na
wengine.
Yapo makundi mengi katika jamii yanayohitaji msaada, mimi
nimetoa mfano mmoja wa vijana tu.
Mtu aliyefanikiwa ni yule aliye BUILD HIS PERSONALITY AND
IMPACT THE WORLD (aliyejijengea uwezo na kuleta mabadiliko chanya ulimwenguni).
Sasa sio lazima uguse ulimwengu wote, fanya kwa kadri ya uwezo wako.
Kama una mali na
hufanyi chochote katika jamii iliyokuzunguka, wewe hujafanikiwa.
Angalizo-Ukisaidia jamii huku wewe unatenda dhambi, bado
haikusaidii, inakua sawa na kumpa Mungu rushwa, yeye hapokei rushwa. Inatakiwa
vitu viwili viende pamoja (yaani usitende dhambi na saidia jamii iliyokuzunguka)
Anza sasa- zaa Matunda.
Be Fruitful
Thanks for the nice message. God blessed you
ReplyDelete