Jinsi kila mmea ulivyo na masharti,kama
vile upandwe ktk aina gani ya udongo, kiwango cha mvua
kinachohitajika
na muinuko mita
ngapi.Vivyo hivyo
Mwanadamu katika kila idara kama ndoa, malezi, uchumi
Ulezi wa mimba n.k ana masharti.Unapokwenda kinyume na
Masharti huwezi pata
matunda mazuri.Masharti haya yanatoka
Kwenye neno la Mungu, neno la Mungu lina nguvu ndilo
linaloshikilia
Angani jua, nyota, mwezi, sayari zingine na ulimwengu
mzima.Neno hilo hilo
Limeshikilia idara mbali mbali katika maisha yako.
(Zaburi 119 :105
Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.)
Fuatilia Mungu anakuelekeza nini kwenye ndoa, malezi n.k
Mfano -Katika malezi anasema mfundishe mtoto njia impasayo
hata iacha
atakapokuwa mtu mzima.Kwa hiyo ukiishia kumuombea tu mtoto
bila kumfundisha ana asilimia kubwa sana ya kupotea.
-Katika ndoa anasema enyi waume wapendeni wake zenu, na wake
watiini waume zenu.maana yake usitegemee ustawi wa ndoa kama neno hili
halitafuatwa.
Hiyo ni mifano michache, endelea kuangalia mambo mengine
katika maisha kama vile kuishi na majirani,maadui, jinsi ya kula n.k. Angalia
Mungu anasemaje na tenda kama Mungu anavyosema, Utapata mafanikio makubwa.
Comments
Post a Comment