Mtu yoyote dunia lazima atakua mfanyakazi wa ufalme mmoja,
shetani au Mungu.Na huwezi kusema mimi hapa dunia simtumikii yeyote, lazima
unakua unatumika sehemu moja ila haujijui.Muda/Time unashikiliwa na kutumiwa na
ulimwengu wa roho wa pande zote mbili tena kwa kuukomboa muda sana.basi ndani
ya muda lazima utakuwa ndani ya ufalme mmoja.Jiulize Dakika tano ulizokaa
ulikuwa unawaza nini, unafanya nini, unasoma nini, unaangalia nini, umevaa
nini, unakunywa nini, una panga nini, unaongea nini, uko maeneo gani,
unakusudia nini n.k kama yoote yanakubalika na Mungu jua hapo unatumikia ufalme
wa Mungu.
(Mathayo 6:24a Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili;
kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na
kumdharau huyu).
Basi rafiki yang komboa muda bado hujachelewa.Kila wakati
uwe mtu wa kujichunguza uko upande gani, kama uko upande mbaya basi unahama
haraka.
Comments
Post a Comment