Skip to main content

Usifanye dhambi makusudi na kutegemea kutubu ni Hatari.


WAEBRANIA 10:26-27
26 Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;
27 bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.

WAEBRANIA 6:4-6
4 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,
5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo,
6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.

Rafiki yangu usitende dhambi kwa makusudi alafu ukasema nitarudi kutubu ni Hatari, Mungu atakuacha bila kujijua.
Hapo nyuma ulitenda dhambi kwa makusudi na kwenda kutubu, Mungu amekusamehe kwa sababu ulikuwa ujafunuliwa neno hili, sasa leo amenena nawe ana kwa ana kupitia neno lake kwa hiyo usirudie tena mchezo huo ni hatari sana. Mungu ni mkali kwenye dhambi, hapendi dhambi anaweza kukuacha bila kujua.
Samson aliachwa bila kujua, wafilisti walipokuja aliinuka apigane nao akitegemea ana nguvu zake kama kwaida (ana MUNGU),  alishangaa anashindwa mpaka wafilisti wakamtoboa macho.
Mbaya zaidi wewe unaweza ukaachwa bila kujua, siku ya mwisho/kifo chako unashangaa unakokwenda ni kwingine (yaani Jehanamu), Unauliza jamani huku ndio Mbinguni –Kilio na kusaga meno.
MUNGU amekuonyesha leo anza upya rafiki yangu.
Maisha ya Duniani ni mafupi sana, ukiishi sana umeishi siku 30,000 ambazo ndio miaka 82.
Maisha baada ya siku 30,000 kama hujafa ni ya taabu tu.Sasa usirudie dhambi tena ili maisha yako ya milele (Yaani Mabilion na mabilioni ya miaka yasiyo na mwisho) yasiwe katika mateso ya moto bali yawe ya FURAHA.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA LUKUKI UNAZOPATA UNAPOOMBA KILA SIKU. (WHY DAILY PRAYER IS IMPORTANT)

Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa-Luka 18:1. i-Unapoomba, ahadi za Mungu alizoziahidi kwako zinatimia. Mungu aliahidi atatutupa Roho mtakatifu, lakini Roho mtakatifu alishuka kwa mitume wakiwa katika kuomba siku kumi. Sehemu nyingine Mungu anasema huwapa thawabu wale wamtafutao. Unapoomba upo katika kitendo cha kumtafuta Mungu, kwa hiyo kuna vitu vingine vizuri huwa anakupa ukiwa unaomba hata kama hujaviomba. Kwa hiyo kama huombi hupati ahadi zako.Kwani shetani anakua na nguvu ya kuzivuruga na kuleta vikwazo. Waebrania 11: 6 – “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”.   ii-Unapoomba ni sawa na binadamu anavyohema kwa kuvuta hewa safi (oxygen) na kutoa nje hewa chafu (cabon), ukiomba unavuta paradiso ndani yako na kutoa nje heeee Dunia, au unamvuta Yesu ndani na kutuoa nje heee ubinadamu.Sasa unapoomba kila siku Yesu

SHARTI LILILOJIFICHA KWA AJILI YA UPONYAJI WA MWILI WAKO.

  Mungu anataka kukuponya lakini ili akuponye shariti lake ni hili; (Warumi 8: 11…Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu)   Unaona sharti hilo- ameanza na neno “Lakini, ikiwa” maana yake hilo ni sharti yaani ukiwa na Roho aliyemfufua Kristo Yesu yaani Roho wa Mungu au Roho mtakatifu ndani yako ndio utapata uponyaji kamili. Lakini kinyume chake hakuna uponyaji.   Sasa kumbe unahitaji kujua utampataje huyo Roho Mtakatifu na kumtunza kwa faida ya Roho na Mwili wako. Maana yake kama hauna huyo uko hatarini. (i)Tubu dhambi zako zote kwa Mungu-Maana Roho mtakatifu anataka awe yeye mwenyewe tu ndani yako. Moyo wako uwe kama karatasi nyeupe isiyokuwa na doa. (ii)Anza kuishi maisha ya kitakatifu kama kutokua na na chuki, kujiinua, hasira, woga, hofu, dharau, kuwaza mambo mabaya yaliyopita au uliyoten

KITU KINACHOMUATHIRI BINADAMU KUTOFIKIA MALENGO YAKE.

Nyumba hujengwa kwa hekima (methali 24:3a) Hapa tunajifunza chocote kinachojengwa ili kifanikiwe kinahitaji Hekima, Bila Hekima chochote hakiwezi jengeka vizuri bali kitakuwa kinaharibiwa. Hapa nakuonyesha vitu vichache ambavyo unavijenga ili vifanikiwe vinahitaji Hekima; -Unajenga ndoa (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga watoto wako wawe wacha Mungu, pia wawe watu wazima wajitegemee na wawe msaada katika taifa (Inahitaji Hekima bila hiyo wanaharibika) -Unajenga kampuni, taasisi, biashara, kikundi, kazi, nchi (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga ujirani mwema (Inahitaji Hekima bila hiyo unaharibika) -Unajenga afya yako(Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Kumjenga au kumfundisha mtu kunataka hekima-bila hivyo utamvuruga kabisa. Hiyo ni mifano ya vitu vichache-lakini kumbuka chochote unachofanya unajenga na kinahitaji hekima. Hekima ni muhimu sana katika maisha yetu, mfalme Sulemani alipoambiwa na Mungu omba chochote aliomba Hekima.