(Mithali 4:23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana
ndiko zitokako chemchemi za uzima).Moyo wako ndio chanzo cha
uzima/maisha/life.Kama ni maji ndio chanzo cha maji hakitakiwi
kuchafuliwa.Hivyo moyo wako unatakiwa kuulinda kuliko chochote (fedha,magari
n.k).Ukiruhusu mabaya katika moyo unakua umeharibu uzima wa kila kitu kama
ndoa,afya,uzima wa roho n.k.
Mabaya unayaruhusu vipi ndani ya moyo wako, ni kwa
kuyatafakari/kuyawaza hapo unakua hujalinda moyo bali unakua umeingiza sumu
kama kunywa maji ya betri.Moyo umeumbiwa kutafakari mambo mazuri tu, yenye
sifa, tena yasiyokuumiza.
Kwa kutafakari mambo mabaya yanayoleta
chuki,hasira,kuhuzunika, kusononeka,kutosamehe,mambo yakupelekea kutenda
dhambi-yamesababisha binadamu kupata magonjwa ya kimwili kabisa kwa sababu chazo
cha uzima (Moyo) kimechafuliwa hivyo kimekuja kinyume cha uzima yaani
mauti.Mfano wa kawaida hasira huleta maradhi ya pumu, kansa, kujiua n.k lakini
pia unakosa uzima wa milele.
(WAFILIPI 4:8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya
kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo
yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo
sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo) Moyo umeumbwa kutafakari vitu kama
vilivyoelezwa hapo juu.ukitafakari kinyume na hapo unakuwa unachafua chanzo
chako cha uzima na kuleta kinyume cha uzima yaani mauti.
(Proverbs 4: 23 And keep watch over your heart with all
care; so you will have life.)
Anza sasa kufanya DIET ya mawazo kama watu wanavyofanya diet
ya chakula ili wawe na afya nzuri kuna baadhi ya vyakula wanaacha.Kwa hiyo na
wewe kila wazo sio la kuwaza.na wewe ambaye umekuwa na mawazo mengi ya
kukuumiza yaliyotokana na watoto,mume,mke,ndugu,mali na kadhalika kuanzia sasa
usielekee kuwaza mawazo hayo, utashangaa mawazo hayo yaletayo machungu yataanza
kuishiwa nguvu pole pole na kupotea.(Kwa kufanya hivyo tunaita unakuwa
unajiscan kama computer inavyo scan virus au unakuwa unaondoa sumu moyoni
kwenye chanzo chako cha LIFE/MAISHA UZIMA.
Moyo pia hautakiwi kuwaza/kutafakari mawazo ya kukupeleke
kutenda dhambi kama uzinzi,ulevi,kutukana,kupigana n.k kwani utakuwa unaukosa
uzima wa roho wa Milele.
Kuanzia sasa anza kukwepa vitu vitakavyopelea moyo kuwaza
mabaya.Kimbiza macho yako kuangalia vitu vibaya, Kimbiza masikio yako
kusikiliza vitu vibaya, kwani mazungumzo mabaya huaribu tabia.
Comments
Post a Comment