Skip to main content

Kuweka wazi udhaifu wa mtu mwingine.


Sifa moja ya mtu mwema/mwenye haki ni kutoweka wazi udhaifu wa mwingine.kutosengenya na kutunza siri za mtu ambazo zikisikika zitamuaibisha muhusika.
(MATHAYO 1:19 Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri).
Hapa Yusufu aligundua mchumba wake ana mimba ambayo yeye hausiki.
akapanga kumuacha kwa siri bila ya mtu mwingine kujua.
Sasa jipime kama wewe una tabia ya kusengenya na kupenda kuweka wazi udhaifu wa mtu mwingine au la, kama una tabia hiyo jirekebishe rafiki yangu.
 pia jihadhari na watu wanao weka wazi udhaifu wa wengine, wala hakuna umuhimu wa mtu mwingine kujua udhaifu huo.watu wa jinsi hiyo wanamapungufu, warekebishe au wakwepe.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA LUKUKI UNAZOPATA UNAPOOMBA KILA SIKU. (WHY DAILY PRAYER IS IMPORTANT)

Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa-Luka 18:1. i-Unapoomba, ahadi za Mungu alizoziahidi kwako zinatimia. Mungu aliahidi atatutupa Roho mtakatifu, lakini Roho mtakatifu alishuka kwa mitume wakiwa katika kuomba siku kumi. Sehemu nyingine Mungu anasema huwapa thawabu wale wamtafutao. Unapoomba upo katika kitendo cha kumtafuta Mungu, kwa hiyo kuna vitu vingine vizuri huwa anakupa ukiwa unaomba hata kama hujaviomba. Kwa hiyo kama huombi hupati ahadi zako.Kwani shetani anakua na nguvu ya kuzivuruga na kuleta vikwazo. Waebrania 11: 6 – “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”.   ii-Unapoomba ni sawa na binadamu anavyohema kwa kuvuta hewa safi (oxygen) na kutoa nje hewa chafu (cabon), ukiomba unavuta paradiso ndani yako na kutoa nje heeee Dunia, au unamvuta Yesu ndani na kutuoa nje heee ubinadamu.Sasa unapoomba kila siku Y...

KITU KINACHOMUATHIRI BINADAMU KUTOFIKIA MALENGO YAKE.

Nyumba hujengwa kwa hekima (methali 24:3a) Hapa tunajifunza chocote kinachojengwa ili kifanikiwe kinahitaji Hekima, Bila Hekima chochote hakiwezi jengeka vizuri bali kitakuwa kinaharibiwa. Hapa nakuonyesha vitu vichache ambavyo unavijenga ili vifanikiwe vinahitaji Hekima; -Unajenga ndoa (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga watoto wako wawe wacha Mungu, pia wawe watu wazima wajitegemee na wawe msaada katika taifa (Inahitaji Hekima bila hiyo wanaharibika) -Unajenga kampuni, taasisi, biashara, kikundi, kazi, nchi (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga ujirani mwema (Inahitaji Hekima bila hiyo unaharibika) -Unajenga afya yako(Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Kumjenga au kumfundisha mtu kunataka hekima-bila hivyo utamvuruga kabisa. Hiyo ni mifano ya vitu vichache-lakini kumbuka chochote unachofanya unajenga na kinahitaji hekima. Hekima ni muhimu sana katika maisha yetu, mfalme Sulemani alipoambiwa na Mungu omba chochote aliomba Hekima....

SIKU ZOTE PENDA KUTUMIA UZOEFU WAKO.

Daudi alikua kijana mdogo lakini alimuua Goriathi jitu kubwa lililowasumbua sana ndugu zake.Wakati anakwenda kupigana nalo watu wake walimdharau na kuona hawezi.Alipong’ang’ania walimvalisha mavazi yao ya vita, lakini yeye aliyavua akaenda kupambana na goriathi kwa kutumia uzoefu wake, Daudi alitumia kombeo na kweli aliweza kumuangamiza goriathi aliyesumbua sana. Kujifunza ni vizuri lakini changanya na uzoefu wako. -Tumia uzoefu wako katika kuendesha ndoa yako japo umeona unaleta matunda ya kuishi vizuri kwa upendo, umoja na amani. Watu wengi ndoa zao zimeharibiwa kwa kutumia uzoefu wa wengine. Unaweza ambiwa wanaume hawafai au wanawake hawafai kumbe wa kwako anafaa. Mfano- mtu mume wake anaposafiri au mke wake anaposafiri anaweza ambiwa na watu wengine kuwa huko mume wako au mke wako alipo atakua si salama anafanya uasherati-hapo anakuwa anapewa uzoefu na watu wengine ambao sio sahihi. Sasa unakuta shuku mbaya zinamuingia mtu na kuleta chuki kati yao. -Hata katika ulaji kuna ...