Mtu mmoja alituhadithia, jana wakati wao wadogo,
walipomtembelea mama yao mdoko, aliwatengea chakula pamoja na watoto wa mama
yake mdogo. wakati wanaendelea kula mama yake mdogo alimkata jicho hilo
(alimtaza vibaya) kiasi kwamba jamaa alishusha tonge chini, alafu mama huyo
akawatazama watoto wake kwa jicho la nyie zubaeni tu ili waongeza speed, lakini akimtaza yeye
ni kwa jicho la kumpunguza speed kula.Jamaa anasema watoto wa huyo mama walikua
sita ila kwa sasa wa kwanza alikufa, wa pili ametolokea nchi za watu hajulikana aliko mpaka leo, watatu
teja yupo nyumbani wa nne na wa tano hawaeleweki shule zimewashinda wapo
nyumbani na wa mwisho ni mdogo. mama huyo hana msaada.
Tunajifuza unapokuwa mchoyo unajilaani wewe na uzao wako.
Unaweza ukawa mchoyo wa mawazo mazuri au mbinu mbalimbali za
maisha kwa jamii inayo kuzunguka.
Wape watu mawazo mazuri ili wafanikiwe, usiwape tu wale wa
karibu unaowajua na kuwapenda.
Jina la mtu halikumbukwi kwa sababu ameacha watoto la hasha linakumbukwa
kwa matendo yake. Majabali wengi duniani tunawakumbuka wao wala watoto wao
hatuwajui.
kwa hiyo zile sababu za nataka nizae niache jina achana nazo
hizo.
upande wako zaaa matendo, gusa maisha ya watu. Bila kugusa
maisha ya watu ukawa unajiishia mwenyewe ni sawa na mti ambao haukuzaa
matunda.yaani wewe unakuwa ni hasara, huna faida yaani hukuzaa na hata kama
ulikuwa na watoto 100.
Upande wa mama yake huyo jamaa- alikuwa fukara lakini
alipotembelewa na wageni alikuwa akiwachinjia kuku wageni hao,watoto wake
waliishia kula vichwa na miguu.lakini mama huyo alipofariki watu walijitokeza
kuwatunza na kuwasomesha baadhi ya watoto wake
(akiwemo yeye anaetuhadisia) hivi sasa anamaendeleo ametembea nchi
mbalimbali , amekuwa wa kuaminiwa na kukubalika, na mtu huyo amekuwa faida kwa
jamii.amekua akifanya semina mbalimbali zenye kugusa maisha ya watu, mambo haya
nimesikia kwenye semina yake jana.baraka amezipata kutoka kwa mama yake, na
watu wote waliobarikiwa jana ni kwa sababu ya mama yake.
Comments
Post a Comment