Kumbukumbu la torati 28:1-8
1 Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa
bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu
wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;
2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti
ya BWANA, Mungu wako.
3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.
4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na
uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo
zako.
5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.
6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.
7 BWANA atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele
yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.
8 BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na
mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA,
Mungu wako.
Comments
Post a Comment