Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa-Luka 18:1. i-Unapoomba, ahadi za Mungu alizoziahidi kwako zinatimia. Mungu aliahidi atatutupa Roho mtakatifu, lakini Roho mtakatifu alishuka kwa mitume wakiwa katika kuomba siku kumi. Sehemu nyingine Mungu anasema huwapa thawabu wale wamtafutao. Unapoomba upo katika kitendo cha kumtafuta Mungu, kwa hiyo kuna vitu vingine vizuri huwa anakupa ukiwa unaomba hata kama hujaviomba. Kwa hiyo kama huombi hupati ahadi zako.Kwani shetani anakua na nguvu ya kuzivuruga na kuleta vikwazo. Waebrania 11: 6 – “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”. ii-Unapoomba ni sawa na binadamu anavyohema kwa kuvuta hewa safi (oxygen) na kutoa nje hewa chafu (cabon), ukiomba unavuta paradiso ndani yako na kutoa nje heeee Dunia, au unamvuta Yesu ndani na kutuoa nje heee ubinadamu.Sasa unapoomba kila siku Y...
Mungu anataka kukuponya lakini ili akuponye shariti lake ni hili; (Warumi 8: 11…Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu) Unaona sharti hilo- ameanza na neno “Lakini, ikiwa” maana yake hilo ni sharti yaani ukiwa na Roho aliyemfufua Kristo Yesu yaani Roho wa Mungu au Roho mtakatifu ndani yako ndio utapata uponyaji kamili. Lakini kinyume chake hakuna uponyaji. Sasa kumbe unahitaji kujua utampataje huyo Roho Mtakatifu na kumtunza kwa faida ya Roho na Mwili wako. Maana yake kama hauna huyo uko hatarini. (i)Tubu dhambi zako zote kwa Mungu-Maana Roho mtakatifu anataka awe yeye mwenyewe tu ndani yako. Moyo wako uwe kama karatasi nyeupe isiyokuwa na doa. (ii)Anza kuishi maisha ya kitakatifu kama kutokua na na chuki, kujiinua, hasira, woga, hofu, dharau, kuwaza mambo mabaya yaliyopi...