Skip to main content

NAKUPENDA –ANASEMA


NAKUPENDA –ANASEMA

(Jifunze hapa chini kama umpendaye unampenda au anakupenda kweli)

Upendo ni nini?-Jibu rahisi Upendo ni Mungu.

Kwa sababu Neno la Mungu/ambalo ndilo MANUAL/KIONGOZI cha mwanadamu linasema- Mungu ni Upendo.

 

Kwa hiyo ili niwe na Upendo lazima niingize program/application ya Upendo ndani yangu ambayo ni Mungu.

Maana yake ili niwe na Upendo lazima niwe na Mungu ndani yangu-kwa sababu yeye ni Upendo.

Maana yake mwenye Upendo ni yule anayejishughulisha kumtafuta Mungu, unapomtafuta Mungu tunaweza sema kwa namna nyingine unatafuta Upendo.

Unaona rafiki yangu-Mungu anakupenda anaanza kukufungua macho.

Kwa maana hiyo basi mtu ambaye hamtafuti Mungu hana Upendo, akisema anakupenda anakudanganya au anakua hajui nini maana ya Upendo.

 

Ndio maana utakuta mtu anayesema anakupenda ndio anayeongea au kukujibu maneno magumu ya kukuumiza moyo au vitendo vya kukuumiza moyo-anapofanya hivyo huo ndio unaitwa uuaji, usipojikinga unakufa kweli, watu wengi wamepata magonjwa ya kufisha kwa sababu ya kuguswa guswa moyo-Uzima huanzia katika moyo wako ndio maana tunaambiwa linda sana moyo wako kuliko vyote ulindavyo maana ndiko chemchem za uzima zitokako.

Ndio maana utakuta watu wanaosema wanapendana ndio wanaogombana au kutalikiana sababu kubwa hawana Upendo.

Mpendwa rafiki endelea kufungua macho yako-kwa hiyo mtu yoyote ambaye hayuko bize kumtafuta Mungu ki kweli kweli (yaani katika roho na kweli-akawa mwabudu halisi) huyo hana Upendo.

 

Hatari ni hii mtu asipokuwa na Upendo – ile sehemu palipotakiwa kukaa Upendo panachukuliwa na chuki (kinyume cha Upendo ni chuki)-Na chuki ni uuaji.

Kwa maana hiyo kama Upendo ni Mungu au Mungu ni Upendo na mtu ili kuupata Upendo lazima afanye installation/kumuuingiza  Mungu ndani yake, Mbaya zaidi watu wengi hawajishughulishi kumtafuta Mungu/Upendo, unaona ni jinsi gani Chuki ilivochukua sehemu kubwa Dunia. Neno la Mungu linasema chuki ni uuaji-yaani yeye amchukiaye ndugu yake ni muuaji, umeona hatari hii?

Kwa mtindo huu- Duniani watu wanatembea sehemu yenye hatari yaani kwenye mavisu, mapanga, misumeno, mabomu, masumu n.k bila ya kujua na kweli wanaangamia.

Basi rafiki anza kumtufuta Mungu sasa ili upate Upendo wa kweli, na uwe balozi wa Upendo kwa kuwafungua macho ndugu jamaa na marafiki-ili Dunia iwe sehemu salama.

1 Waraka  wa Yohana 5:8  (Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo). Unaona maana ya mstari huu ni ili uwe na Upendo lazima umjue Mungu/ndio kule kumtafuta. Na pia mstari umemalizia kusema Mungu ni Upendo- yaani Upendo ni Mungu,kwa hiyo ili uwe na Upendo lazima  umuingize Mungu ndani yako.

 

Angalia siri hii-Unajua unaweza ukatoa vitu na kuwapa masikini lakini ukawa huna Upendo, neno hilo limenenwa 1Wakoritho 13:3.

Mtu anaweza akakuletea zawadi nzuri kwenye harusi yako, au akaja msibani na kusaidia sana au akaja hospitalini kukuona na kukuletea chakula lakini akawa hana Upendo.Akitoka hapo akaendelea kukusema vibaya na kukutakia mabaya.Kwa kusema hivi sio uache kutenda mema-hapana Mungu anatutaka sana tutende mema ila katika Upendo-anasema yote yafanyike kwa Upendo-Let Love Lead.

Wengine katika harusi zao waliletewa zawadi kumbe ilikua mabomu ya kuwafunga kizazi-unaona hatari hii.Ilikua kama ni jambo la upendo kumbe hakuna upendo.

Mungu anakupenda sana ndio maana yeye mwenyewe anakupa siri hii/anakufungua macho yako-anza kumtafuta Mungu kwa bidii ili upate Upendo.

Kumtafuta Mungu ni pamoja na kuacha Ubaya.Sifa ya Upendo haufurahii Ubaya wa aina yoyote-Kama unafurahia Ubaya bado huna Upendo.

 

Ni kwamba-pokea siri hii nakunong’oneza-Mauti itakapokukuta, Upendo ndio KEY/funguo au tiketi ya kuingia Mbinguni na kuishi maisha mazuri ya raha milele. Kwa sababu utakua umekufa na Mungu/Upendo, utakua umekufa na nia ya Mungu, kusudi la Mungu, Muelekeo wa Mungu.

 “Heri wafu wafao katika Bwana” yaani wana heri wale waliokufa/wamelala wakiwa na Upendo maana ndio nia ya Mungu, kusudi la Mungu, Muelekeo wa Mungu.Ila watakaokufu/lala huku hawana Upendo (nia,kusudu,mwelekeo wa Mungu) hao ole kwao imesimama-ole ni kinyume cha heri na ni neno linaloashiria mabaya.Ufunuo 14:13.

Mungu hataki tena kuja kukaa na kuishi milele na roho iliyo kinyume na yeye kwani itamsumbua.Kiongozi yoyote anapenda watu ambao wanatawalika ili wasimsumbue katika utawala wake.Mungu naye kama mfalme anataka akutawale . 

 

Basi ilikua katika kuonyeshana, kufumbuana macho - basi rekebisha palipo pungua. Nakupenda sana.

www.mtibora.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA LUKUKI UNAZOPATA UNAPOOMBA KILA SIKU. (WHY DAILY PRAYER IS IMPORTANT)

Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa-Luka 18:1. i-Unapoomba, ahadi za Mungu alizoziahidi kwako zinatimia. Mungu aliahidi atatutupa Roho mtakatifu, lakini Roho mtakatifu alishuka kwa mitume wakiwa katika kuomba siku kumi. Sehemu nyingine Mungu anasema huwapa thawabu wale wamtafutao. Unapoomba upo katika kitendo cha kumtafuta Mungu, kwa hiyo kuna vitu vingine vizuri huwa anakupa ukiwa unaomba hata kama hujaviomba. Kwa hiyo kama huombi hupati ahadi zako.Kwani shetani anakua na nguvu ya kuzivuruga na kuleta vikwazo. Waebrania 11: 6 – “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”.   ii-Unapoomba ni sawa na binadamu anavyohema kwa kuvuta hewa safi (oxygen) na kutoa nje hewa chafu (cabon), ukiomba unavuta paradiso ndani yako na kutoa nje heeee Dunia, au unamvuta Yesu ndani na kutuoa nje heee ubinadamu.Sasa unapoomba kila siku Y...

SHARTI LILILOJIFICHA KWA AJILI YA UPONYAJI WA MWILI WAKO.

  Mungu anataka kukuponya lakini ili akuponye shariti lake ni hili; (Warumi 8: 11…Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu)   Unaona sharti hilo- ameanza na neno “Lakini, ikiwa” maana yake hilo ni sharti yaani ukiwa na Roho aliyemfufua Kristo Yesu yaani Roho wa Mungu au Roho mtakatifu ndani yako ndio utapata uponyaji kamili. Lakini kinyume chake hakuna uponyaji.   Sasa kumbe unahitaji kujua utampataje huyo Roho Mtakatifu na kumtunza kwa faida ya Roho na Mwili wako. Maana yake kama hauna huyo uko hatarini. (i)Tubu dhambi zako zote kwa Mungu-Maana Roho mtakatifu anataka awe yeye mwenyewe tu ndani yako. Moyo wako uwe kama karatasi nyeupe isiyokuwa na doa. (ii)Anza kuishi maisha ya kitakatifu kama kutokua na na chuki, kujiinua, hasira, woga, hofu, dharau, kuwaza mambo mabaya yaliyopi...

KITU KINACHOMUATHIRI BINADAMU KUTOFIKIA MALENGO YAKE.

Nyumba hujengwa kwa hekima (methali 24:3a) Hapa tunajifunza chocote kinachojengwa ili kifanikiwe kinahitaji Hekima, Bila Hekima chochote hakiwezi jengeka vizuri bali kitakuwa kinaharibiwa. Hapa nakuonyesha vitu vichache ambavyo unavijenga ili vifanikiwe vinahitaji Hekima; -Unajenga ndoa (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga watoto wako wawe wacha Mungu, pia wawe watu wazima wajitegemee na wawe msaada katika taifa (Inahitaji Hekima bila hiyo wanaharibika) -Unajenga kampuni, taasisi, biashara, kikundi, kazi, nchi (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga ujirani mwema (Inahitaji Hekima bila hiyo unaharibika) -Unajenga afya yako(Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Kumjenga au kumfundisha mtu kunataka hekima-bila hivyo utamvuruga kabisa. Hiyo ni mifano ya vitu vichache-lakini kumbuka chochote unachofanya unajenga na kinahitaji hekima. Hekima ni muhimu sana katika maisha yetu, mfalme Sulemani alipoambiwa na Mungu omba chochote aliomba Hekima....