Nyumba hujengwa kwa
hekima (methali 24:3a)
Hapa tunajifunza chocote kinachojengwa ili kifanikiwe kinahitaji
Hekima,
Bila Hekima chochote hakiwezi jengeka vizuri bali kitakuwa
kinaharibiwa.
Hapa nakuonyesha vitu vichache ambavyo unavijenga ili
vifanikiwe vinahitaji Hekima;
-Unajenga ndoa (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika)
-Unajenga watoto wako wawe wacha Mungu, pia wawe watu wazima wajitegemee na wawe
msaada katika taifa (Inahitaji Hekima bila hiyo wanaharibika)
-Unajenga kampuni, taasisi, biashara, kikundi, kazi, nchi
(Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika)
-Unajenga ujirani mwema (Inahitaji Hekima bila hiyo unaharibika)
-Unajenga afya yako(Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika)
-Kumjenga au kumfundisha mtu kunataka hekima-bila hivyo
utamvuruga kabisa.
Hiyo ni mifano ya vitu vichache-lakini kumbuka chochote unachofanya
unajenga na kinahitaji hekima. Hekima ni muhimu sana katika maisha yetu, mfalme
Sulemani alipoambiwa na Mungu omba chochote aliomba Hekima.
Kama unahitaji Hekima huombwa kwa Mwenyezi Mungu-maana
Hekima ni roho
Pia kitu kingine cha kunogesha zaidi kitu unachojenga, au
kukunogesha wewe mwenyewe maana unajijenga ni MAARIFA. Mithali 23:4 “Na
kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza”.
Kwa hiyo vitu nilivyokutajia hapo juu pamoja na wewe
mwenyewe ili vinoge zaidi ni kuongeza Maarifa.Maana yake ongeza uwezo katika
jambo lako lolote kati ya hayo niliyotaja juu (japo maarifa ni roho pia).Iwe
biashara, kampuni, shamba, watoto, ndoa n.k endelea kujifunza katika njia
zinazokubalika na Mungu jinsi gani uboreshe, bila hivyo utasimama hapo hapo.
Neno linasema “Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo”-
Mithali 23:5b.
Tumejifunza ni kwa namna gani kuanzia sasa mambo yetu ya
aina yoyote jinsi tutakavyo yajenga.Na umejionea mwenyewe ni wapi ulipotumbukia.
Comments
Post a Comment