Skip to main content

SHARTI LILILOJIFICHA KWA AJILI YA UPONYAJI WA MWILI WAKO.

 

Mungu anataka kukuponya lakini ili akuponye shariti lake ni hili;

(Warumi 8: 11…Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu)

 

Unaona sharti hilo- ameanza na neno “Lakini, ikiwa” maana yake hilo ni sharti yaani ukiwa na Roho aliyemfufua Kristo Yesu yaani Roho wa Mungu au Roho mtakatifu ndani yako ndio utapata uponyaji kamili. Lakini kinyume chake hakuna uponyaji.

 

Sasa kumbe unahitaji kujua utampataje huyo Roho Mtakatifu na kumtunza kwa faida ya Roho na Mwili wako. Maana yake kama hauna huyo uko hatarini.

(i)Tubu dhambi zako zote kwa Mungu-Maana Roho mtakatifu anataka awe yeye mwenyewe tu ndani yako. Moyo wako uwe kama karatasi nyeupe isiyokuwa na doa.

(ii)Anza kuishi maisha ya kitakatifu kama kutokua na na chuki, kujiinua, hasira, woga, hofu, dharau, kuwaza mambo mabaya yaliyopita au uliyotendewa, masengenyo, kunenea wengine mabaya n.k.

Roho mtakatifu hataki kabisa kuchangamana na vitu hivyo anataka awe peke yake. Ndio maana Roho mtakatifu anaweza kukushukia na kuondoka ukiingiza mambo mabaya ambayo wengi huita dhambi ndogo. Watu wengi hufikiri dhambi ni uzinzi, ulevi na uuaji, vingine huona sio dhambi bali ni dhambi ndogo, hapana mtu wa Mungu usibague dhambi kubwa na ndogo, ukaharalisha dhambi unazoona ndogo Roho mtakatifu anaoondoka, akiondoka nani atahuisha mwili wako.

 Roho mtakatifu anataka moyo wako uwe mweupe kama karatasi/plain paper ndio anakaa, anataka awe yeye peke yake. Anza sasa kuachilia mambo mabaya uliyoshikilia moyoni ili moyo wako uwe mweupe kama karatasi, Roho mtakatifu akae ndani yako upate uponyaji kamili, na pia afanye na wewe kazi nyingine.

Neno kutoka (Mithali 4:23 linasema “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima”)

Unaona neno hilo! Ukiulinda moyo wako ukawa mweupe zitatoka chemchemi za uzima-yaani Roho mtakatifu atakukalia na utapata uzima wa mwili KABISA KABISA na Roho yako.

 

Waumini wengi hivi sasa wanasumbuliwa na magonjwa na hawaponi kwa sababu ya kutenga dhambi kubwa na ndogo, Roho mtakatifu hataki kabisa ndio maana anaitwa MTAKATIFU ni msafi hataki mawaa/uchafu wa dhambi aina yoyote.

Roho mtakatifu anakaa kwenye UPENDO – Neno linasema mambo yote yafanyike kwa Upendo na pia inatakiwa Imani itendayo kazi kwa upendo.

Imani inayotenda kazi bila Upendo sio Imani sahihi – roho mtakatifu hayupo humo sasa nani atahuisha mwili wako akuponye magonjwa?

 Imani ziko nyingi hata wapagani wana Imani. (Wagalatia 5:6c – bali Imani itendayo kazi kwa upendo/but faith which worketh by love)

 

 Unasikia mtu wa Mungu, kuanzia sasa acha kumwabudu Mungu huku;-

-unamchukia mwenzako-Roho mtakatifu hakai kwako, na huwezi kupona.

-Acha kudharau, unajiona bora kuliko mwenzako-Roho mtakatifu hakai kwako, na huwezi kupona.

- Acha kumwabudu Mungu huku unaona kanisa lako ndio bora kuliko wengine, yaani hao wana dhambi Roho mtakatifu hatakaa kwako, na huwezi kupona. Tumeambiwa tusikuhukumu, hata yohana 3:16-17 inaeleza kuwa Yesu alikuja  kuukomboa ulimwengu na sio KUUHUKUMU Ulimwengu.

-Acha kuweka kisasi moyoni -Roho mtakatifu hakai kwako, na huwezi kupona.

-Acha kujiinua na kujiona super star kwa karama uliyokirimiwa na Mungu-Roho mtakatifu ataondoka kwako na utabaki mtupu.Hatari ni kwamba karama yako itaanza kutumiwa na shetani.Siku zote Mungu akikupa karama alafu ukamwacha Mungu, yeye huwa hachukui karama ila ROHO MTAKATIFU hakuachii lazima aondoke alafu inaingia roho mbaya.Kama ulikuwa na karama ya Unabii utakuwa mchawi, kama ulikua unaimba nyimbo za Mungu utahama taratibu utaanza kuimba nyimbo za shetani au kuingiza staili za shetani katika Nyimbo zako (Iwe uchezaji n.k).Hakuna super star kwenye mambo ya Mungu ukiona hali hiyo inaingia pambana nayo.Ili Roho mtakatifu asikuache na upate uponyaji kamili.

-Acha kumwabudu Mungu huku una woga, unaishi na wasi wasi kuhusu ndoa yako, mali yako na kadhalika-Roho mtakatifu hakai, na huwezi kupona.

Neno linasema (Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.1 Timotheo 7). Kwa hiyo ukiwa na woga woga hiyo ni roho nyingine, kumbuka roho mtakatifu anataka akae peke yake, hakai na kingine anaondoka.

Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.

-Acha kumwabudu Mungu huku una kiburi, tamaa, wivu wa aina yoyote -Roho mtakatifu hakai, na huwezi kupona.

-Madhambi mengine ambayo sijayataja yako dhahiri sana nayo Roho mtakatifu hachangamani nayo; uzinzi, ulevi, husuda, uchafu, uaji,uchawi, ibada ya sanamu, ugomvi, wizi n.k soma pia wagalatia 5:19-20 utaona madhambi yametajwa hapo.

 

Kumbuka somo hili ni ili uweze kupata uponyaji kamili lazima uwe na Roho mtakatifu ndani ili akuhuishe mwili wako.Sasa mtu wa Mungu hayo machache yaliyotajwa hapo juu Roho mtakatifu hapatani nayo na hakai kwa mtu anayeishi na mambo hayo, Je utapona magonjwa yako kama yeye hayupo?

Hata Yesu alipokuwa akiwaponya watu aliwaambia umesamehewa dhambi maana yake walisafishwa, na kisha hata kama yeye aliwaponya masharti ilikuwa USITENDE DHAMBI tena lisije likakupata jambo lililobaya zaidi.

Sasa anza kutubia dhambi zako zote hapo hapo ulipo, hata kama ulikuwa mchungaji umeyasema makanisa mengine vibaya, una chuki, tubia ili Roho mtakatifu akushukie, iwe muumini unachukia wengine, wivu, masengenyo, kuwawazia wengine mabaya, kupenda usikie mwenzako kapatwa na mabaya n.k tubia hapo hapo ili Mungu/Roho mtakatifu afanye makao ndani yako na kupata uponyaji wa kweli sio wa kipindi tu.

Wewe nae mwingine ambaye hata kanisa hulijui tubia dhambi zako zote hapo hapo ili Mungu/Roho mtakatifu afanye makao ndani yako na kupata uponyaji wako na pia kuwa na uzima wa milele.

 

(iii)Uwe mwenye kusoma Neno la Mungu hicho ndicho chakula cha Roho mtakatifu-kwa kufanya hivyo utaendelea kumtunza ndani yako.

(Mathayo 4:4 - Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu).

Kama husomi neno la Mungu utakufa-jitahidi kusoma neno la Mungu.

Hakikisha kila siku unapata neno la Mungu, kama unavyohakikisha unakula chakula.Uko makini kumtunza mtu wa nje-asubuhi chai, mchana, na chakula cha usiku.Lakini unamsahau mtu halisi wa ndani kumtunza kwa kumpa chakula chake, unaona sasa mwili wako wa nje unakufa kwa sababu huyo wa ndani ndio muhimili wako.

Wewe mwenyewe umejiona-uliposoma hii makala fupi kuna uhai umepata, kuna nguvu umepata-sasa uhai uliopata na hizo nguvu unaweza ziongeza mara elfu nyingi, ni juhudi yako mwenyewe. Nguvu nyingi, na uzima tele umeziacha mwenyewe.

 

(iii)Uwe muombaji ili usije ukajaribiwa ukarudi kwenye machafu uliyoyatubu, ukamtenda Mungu dhambi, kumbuka yeye ni mtakatifu hakai kwenye dhambi.

Pia kumbuka yeye ni Roho ambaye unataka akae ndani yako ili upate uponyanyi wa mwili wako na uzima wa milele.

(Mathayo 26:41 - Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu).

www.mtibora.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA LUKUKI UNAZOPATA UNAPOOMBA KILA SIKU. (WHY DAILY PRAYER IS IMPORTANT)

Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa-Luka 18:1. i-Unapoomba, ahadi za Mungu alizoziahidi kwako zinatimia. Mungu aliahidi atatutupa Roho mtakatifu, lakini Roho mtakatifu alishuka kwa mitume wakiwa katika kuomba siku kumi. Sehemu nyingine Mungu anasema huwapa thawabu wale wamtafutao. Unapoomba upo katika kitendo cha kumtafuta Mungu, kwa hiyo kuna vitu vingine vizuri huwa anakupa ukiwa unaomba hata kama hujaviomba. Kwa hiyo kama huombi hupati ahadi zako.Kwani shetani anakua na nguvu ya kuzivuruga na kuleta vikwazo. Waebrania 11: 6 – “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”.   ii-Unapoomba ni sawa na binadamu anavyohema kwa kuvuta hewa safi (oxygen) na kutoa nje hewa chafu (cabon), ukiomba unavuta paradiso ndani yako na kutoa nje heeee Dunia, au unamvuta Yesu ndani na kutuoa nje heee ubinadamu.Sasa unapoomba kila siku Y...

KITU KINACHOMUATHIRI BINADAMU KUTOFIKIA MALENGO YAKE.

Nyumba hujengwa kwa hekima (methali 24:3a) Hapa tunajifunza chocote kinachojengwa ili kifanikiwe kinahitaji Hekima, Bila Hekima chochote hakiwezi jengeka vizuri bali kitakuwa kinaharibiwa. Hapa nakuonyesha vitu vichache ambavyo unavijenga ili vifanikiwe vinahitaji Hekima; -Unajenga ndoa (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga watoto wako wawe wacha Mungu, pia wawe watu wazima wajitegemee na wawe msaada katika taifa (Inahitaji Hekima bila hiyo wanaharibika) -Unajenga kampuni, taasisi, biashara, kikundi, kazi, nchi (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga ujirani mwema (Inahitaji Hekima bila hiyo unaharibika) -Unajenga afya yako(Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Kumjenga au kumfundisha mtu kunataka hekima-bila hivyo utamvuruga kabisa. Hiyo ni mifano ya vitu vichache-lakini kumbuka chochote unachofanya unajenga na kinahitaji hekima. Hekima ni muhimu sana katika maisha yetu, mfalme Sulemani alipoambiwa na Mungu omba chochote aliomba Hekima....