Ni
kwamba kuna mafanikio makubwa sana ukiwa unatumia silaha ya UMOJA na UPENDO.
Zab 133:1-3 "Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza,
Ndugu wakae pamoja, kwa umoja.
Ni kama mafuta mazuri kichwani,
Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni,
Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.
Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni.
Maana ndiko BWANA alikoamuru baraka,
Naam, uzima hata milele".
-Ukivitumia
vitu hivi maandiko yanasema hujenga BOMA zuri kwao.
Yaani
kuna kuwa na uzio mzuri ambao adui hawezi kupita na kushambulia Ndoa yako,
taasisi yako, miradi yako, familia yako n.k.
(i)Kwa hiyo tumia Umoja na Upendo kujenga
Boma zuri katika miradi yako (Hakikisha wafanya kazi wako unawajenga katika
Umoja na Upendo ili kuwe na Boma zuri adui asivamie mradi wako. Hakikisha nawe
kama kiongozi wa mradi usiwachukie baadhi ya wafanya kazi wako, maana nao
watakuchukia na kuharibu Boma lako, ndio maana unakuta kuna wengine wanatoa
siri ya shirika lako,mradi wako au wanakuibia n.k ni kwa sababu hakuna Umoja na
Upendo kwa hiyo Boma linakua limeharibika.Kuwa makini asilimia kubwa ya watu
utakao wachukia nao watakuchukia, labda watu wachache sana wenye hatua ya juu
sana ya Imani ndio watakao kupenda.Kwa hiyo usiwe mwepesi kuchukia watu)
(ii)Wanandoa
hakikisha mnatumia silaha hii ya Umoja na Upendo ili muwe katika Boma zuri.Umoja sio kukaa
pamoja tu-kwani mnaweza kukaa pamoja lakini hamna umoja.Umoja ni kwamba NIA zenu,
MISIMAMO, MAWAZO yenu yakubaliane, bila hivyo hakuna umoja hata kama mnalala
kitanda kimoja na hivyo Ndoa yenu au familia yenu inakuwa haina BOMA zuri muda
wowote adui anaingia.Pia nia zikiwa tofauti ndio uchawi wenyewe mnakua
mnalogana wenyewe kwa sababu mna migogoro/conflict katika ulimwengu wa roho
ambao ndio NIA, FIKRA, MAWAZO na kila mtakulokua mnatenda halitafanikiwa-utaona
jambo linaenda kama linafanikiwa na baadae linazimika au kuleta madhara makubwa
na sehemu nyigine kupelea Mauti kabisa. Wanandoa pia msifichane mambo, mkiona
mumefikia huko mko katika hatua mbaya-rudini tengenezeni haraka. Ndugu mpendwa
hakikisha katika Ndoa yako usikubali Umoja na Upendo kuondoka, kubalianeni,
shukeni na kukubaliana mpaka ndani ya NIA zenu bila hivyo ni sawa na
kijinyonga.
-UMOJA
na UPENDO hufanya mahali pawe pazuri, sio mali inayofanya mahali pawe pazuri.
Mtunzi
wa Tenzi 140-Anasema “Mahali ni pazuri ndugu wanapokaa, wakipata vema na
wakipendana”
Kwa
hiyo mkipatana vema katika nia zenu na kupendana-Pahari hapo, iwe ndoa,
taasisi, kampuni panakuwa pazuri, yaani eneo hilo linafanikiwa kwa ujumla
katika pande zote (Yaani panakuwa na uchumi mzuri, afya nzuri,mume mzuri, mke
mzuri, watoto wazuri, chakula kizuri, uzima- hakuna vifo vya hovyo hovyo katika
familia, amani, haki n.k)
Na
kwenye taasisi ni hivyo hivyo kunakuwa na uchumi mzuri, afya nzuri,bosi mzuri,
wafanyakazi wazuri, matokeo mazuri,uzima-hakuna vifo vya hovyo hovyo katika
taasisi, amani, haki n.k
Tumia
silaha hii ya Umoja na Upendo katika maeneo yako yote-usipende kuwa mwepesi wa
chuki na magomvi-Solution/Ufumbuzi wako mkubwa wa matatizo katika kila eneo iwe
ni kujenga Umoja na Upendo.
Kama
kuna mtu katika taasisi/biashara yako/ familia yako awe ndugu unayemlea umetumia
jitihada kubwa pamoja na maombi kumleta katika Umoja na Upendo haelekei
muondoe-kwani atatengeneza tundu katika Boma lako na adui kukuvamia, pia huyo
atakua anakuloga kwa sababu NIA yake haiendani na wewe. Kama ni ndugu haeleweki
ni vyema uwe unamsaidia kwa mbali, ila usikae nae karibu.
Kwani
maandiko yanasema Mathayo 10: 36 “na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake”
-Wewe
unaeanzisha mradi hakikisha uwe na maono ya kuwa na watu wakufanya nao pamoja
ili uwe katika Boma zuri.Usiwaze kuwa peke yako milele-hutafika mbali.Hata
wataalamu wa biashara wanasema mtu anayefanya mradi peke yake atakwenda haraka
ila hafiki mbali, bali wanaofanya kama timu watakwenda taratibu ila watafika
mbali.
Kuna
Nguvu katika Umoja na Upendo-ila uwe makini kuchagua timu nzuri.Yesu alilijua
hilo ndio maana alichagua timu ya kusaidiana nae wale mitume kumi na mbili,
alikuwa makini kabla ya kuwachagua aliomba sana usiku.Kuwa makini kuchagua wafanyakazi,
marafiki hata mume au mke wa kuoa.
Usikulupuke
kuoa na usikulupuke kuolewa.
Yesu
alitambua sana umuhimu wa Umoja, katika nyakati zake za mwisho alituombea
Umoja.
Yohana
17:11-“Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja
kwako, Baba mtakatifu, kwa jina lako uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.
Unaona
kuna siri kubwa katika Umoja hapa Yesu ametuombea umoja na tunagundua kumbe
naye/Yesu na Mungu baba walikuwa na umoja ndio maana UTUKUFU mkubwa ulionekana Dunia.
Ukitaka
UTUKUFU uonekane katika maeneo yako yote ya ndoa, kazi, biashara, taasisi,
familia, ndugu, ukoo, kikundi n.k
Tumia
silaha hii ya UMOJA na UPENDO.
www.mtibora.blogspot.com
Comments
Post a Comment