Unapoambiwa
chukua tahadhari-nia ni kuepuka majanga.
Kuna
mambo ambayo tumeambiwa kuchukua tahadhari ila unayapuzia au wengine hawayajui.Baadhi
ya mambo ambayo nimejaliwa kukuletea ni haya mawili;
(i)
“Jihadharini
na wanadamu…” Mathayo 10:17a
(ii)
“Jihadharini na manabii wa uongo, watu
wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali” Mathayo 7:15
Nawatambuaje?
Sasa
jinsi ya kuwatambua hawa wanadamu hatari/ndugu wa uongo/mbwa mwitu, Pamoja na
manabii wa uongo ni rahisi sana, wala haiitaji uwe mtu wa karama fulani au nabii.
Jinsi
ya kuwatambua ni kuangalia matendo yao kwa macho kabisa ya kibinadamu ambayo
unayo.
(Mathayo 7:16 &18
Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini
katika mibaruti?
18
Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.)
Unaona
utakua unaona matendo yao, mtu mwema hawezi kufanya matendo maovu, pia mtu
mbaya hawezi kufanya matendo mema. Mtu mbaya ataigiza igiza matendo mazuri
ndio kuvaa mavazi ya Kondoo lakini ndani ni mbwa mwitu, siku moja atakutolea
undani wake/uumbwa mwitu ndio majanga yanapokukuta-ndio maana utakuta mtu
anakuambia hunijui eee, yaani humjui kuwa mbwa mwitu. Wengine huwa wanasema
nitakutolea uvivu, yaani uumbwa mwitu. Ni sawasawa na kufuga Simba-siku
nyingine unakua unacheza naye, ila siku akikutolea usimba ni majanga.waliofuga
Simba baadhi yao waliuuwa na Simba wao na wengine kukoswa koswa.
Ndio
maana bado tunasisitiziwa “Na adui za mtu ni
wale wa nyumbani mwake.” Mathayo 10:36.
Kuanzia
sasa mtu yeyote, awe rafiki yako, jirani yako, baba yako, mama yako, mwalimu
wako, dada, kaka, mjomba, shangazi, babu, bibi, bosi, mtoto wako mchungaji
wako, na yeyeyote anayejiita nabii, mtathimini matendo yake kujua kama ni mbwa
mwitu au ni nabii wa uongo.
-Mtu
huyu anaishije na jamii iliyo mzunguka kama majirani zake, je anawapenda au ni
mtu wa ugomvi ugomvi, mkali mkali, ana chuki amekunja kunja uso, siri ni kwamba roho
iliyondani ya mtu unaweza ichungulia haraka kupitia uso wa mtu ulivyo, macho
yake yalivyo na vitu vingine kama matendo, ongea, mavazi, utembeaji n.k.Kaini
kabla ya kumuua ndugu yake Habili, Mungu aliona uso wake, akamwambia mbona uso
wako umekunjamana-akamwambia iko dhambi mbele inakuotea. Sasa unapomtathimini mtu ukiona kadosari hata
kadogo weka alama kubwa ya kiulizo. (“Yeyote aliye
mwaminifu katika mambo madogo, atakuwa mwaminifu katika mambo makubwa; na
yeyote asiye mwaminifu katika mambo madogo, hatakuwa mwaminifu katika mambo
makubwa”-Luka 16-10)
-Pili,
Mtu huyu anaishije na familia yake yaani mke wake, mume wake, watoto wake-Je
ametelekeza, ana amani nao. Ukiona ipo shida kaa nae kwa makini/chukua
tahadhari hata kama ni bosi wako.
-Tatu, Mtu huyu anaishije katika mazingira ya kazi, kikundi, taasisi,ukoo, chama
au biashara-ukiona ni mgomvi mgomvi, matusi, yeye ni chanzo cha matatizo migogoro katika
kila eneo-mtu huyo jihadhari nae.
-Nne,
Ukiona mtu mzinzi, ana tamaa tamaa kila kitu akiona anatamani,ana tamaa sana ya
pesa, mshirikina-uwe makini/jihadhari nae.
(1
wakoritho 5:11 Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu
aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au
mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye).
Najua
ukitulia bado unaweza pata mambo mengine:-
Madhara
gani unaweza kuyapata usipochukua tahadhari-
Kwa
sababu watu wanaofanya matendo ya jinsi hiyo wako kwenye utawala wa shetani-na
shetania nia yake ni mauti/kuua kwa hiyo usipochukua tahadhari
Ndoa
yako yaweza kuuliwa, watoto wako, uchumi wako, kampuni yako, elimu yako, kazi
yako, biashara yako, afya yako, mwili wako kufa kabisa na roho yako kukosa uzima
ya milele.
(Mwivi haji ila aibe na kuchinja na
kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele – Yohana 10:10)
-Ndio maana unakuta sehemu nyingine
mchungaji kabisa katembea na mke wa mtu-tatizo mume hakuchukua tahadhari, au
mke hakuchukua tahadhari au walikutana wote mchungaji na huyo mke wa mtu wote
wameharibika/wameoza/ni mbwa mwitu/ni ndugu wa uongo/ni manabii wa uongo kwa
hiyo wakakubaliana.
-Au unakuta kaka anambaka mtoto wa dada
yake.
Watu wa jinsi hii huwa haitokei tu
lakini huwa anakua na viashiria ambavyo vinaonyesha huyu ni mbwa mwitu, ndugu
wa uongo au nabii wa uongo.
Hiyo ni mifano michache ila yako mambo
mengi mabaya ambayo watu wametendewa kwa sababu ya kutochukua tahadhari.
“Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa
maarifa” Hosea 4:6a.
Kuanzia sasa mtu yoyote mfanyie
interview kwa kumpima-usikubali kuwa karibu au kujiunganisha na mtu bila kumpima
na kuona kama anafaa kuwa karibu na wewe.
Hata mashirika au taasisi mbalimbali kabla
ya kumuajili mtu, humpima yaani kumfanyia interview kama anafaa, na baada ya
hapo hata akionekana anafaa humpa miezi mingine michache ya kumuangalia kama
anafaa, akivuruga wanamuondoa.
Unaona hatari hii –sasa unapoendelea
kuangalia upande wa pili, endelea kujitathmini na wewe, je na mimi nina tabia
hizi ambazo hazikubaliki-basi unajirekebisha kabla watu hawajachukua tahadhari
dhidi yako.Ndio maana kuna watu wengine- watu wanachukua taadhari ya
kuwakopesha fedha, wanaambiana usimkopeshe huyo.lakini kumbe bado yako mambo
mengi ya kuchukua taadhari.
Nifanye
nini ili kuchukua tahadhari?
Inategemeana na hali utakayoiona
mwenyewe na kuchukua baadhi ya njia hizi chini, japo unaweza pata njia nyingine
zaidi;
i-Kujitenga
na watu wa jinsi hii.
1
wakoritho 5:11 Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu
aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au
mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.
ii-Kuwa
na busara na kuwa mpole.
-Mathayo
10:16 “Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na
busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua”.
-Mathayo 5:5 “Heri walio wapole, maana
watairithi nchi”.
iii-Kuombea.
-Yakobo 5:16b “ kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa
sana, akiomba kwa bidii”.
Muombee huyo mtu mwenye shida hiyo abadilike.Kemea pepo linalomsumbua na kuwa na tabia hiyo isiyofaa mpaka limuachie huru.
iii-Peleka
habari njema.
Ukiona watu hao wanaweza kukusikiliza
waambie habari njema, wengine wanafanya kwa kutokujua, wape mwanga wapo baadhi
au wote wanaweza geuka na kuwa wazuri na sio Mbwa mwitu
-Yohana 17:17 “Uwatakase kwa ile kweli;
neno lako ndiyo kweli”
Maneno yanatakasa yanamtenganisha mtu na roho chafu zinazomuandama.
Comments
Post a Comment