Daudi alikua kijana mdogo lakini alimuua
Goriathi jitu kubwa lililowasumbua sana ndugu zake.Wakati anakwenda kupigana
nalo watu wake walimdharau na kuona hawezi.Alipong’ang’ania walimvalisha mavazi
yao ya vita, lakini yeye aliyavua akaenda kupambana na goriathi kwa kutumia
uzoefu wake, Daudi alitumia kombeo na kweli aliweza kumuangamiza goriathi
aliyesumbua sana.
Kujifunza
ni vizuri lakini changanya na uzoefu wako.
-Tumia
uzoefu wako katika kuendesha ndoa yako japo umeona unaleta matunda ya kuishi
vizuri kwa upendo, umoja na amani. Watu wengi ndoa zao zimeharibiwa kwa kutumia
uzoefu wa wengine. Unaweza ambiwa wanaume hawafai au wanawake hawafai kumbe wa
kwako anafaa. Mfano- mtu mume wake anaposafiri au mke wake anaposafiri anaweza
ambiwa na watu wengine kuwa huko mume wako au mke wako alipo atakua si salama
anafanya uasherati-hapo anakuwa anapewa uzoefu na watu wengine ambao sio sahihi.
Sasa unakuta shuku mbaya zinamuingia mtu na kuleta chuki kati yao.
-Hata
katika ulaji kuna vyakula vingine vile ambavyo vinakubalika, vinafaa kwa watu
wengine lakini kwa wengine haviwafai-Mfano kuna mtu mwingine akinywa maziwa
yanamfaa katika tumbo lake, ila kuna mwingine hayamfai yanamuumiza tumbo. Kwa
hiyo anayeumizwa tumbo lake atasema maziwa ni mabaya kumbe kwa mwingine ni
mazuri.
Kwa
hiyo Duniani kuna vitu vingi ambavyo vinaweza visifae kwa mwingine ila kwa
mwingin vinafaa.
Endelea kujifunza kuujulia mwili wako, kazi
yako, biashara yako, ndoa yako n.k
Nyongeza-Wakati
mwingine kwa kutojijua unaweza ukawa unakunywa dawa bure kumbe ungeishi kwa
mtindo mwingine usingekuwa unakunywa dawa.Mfano unaweza ukawa unakunywa dawa za
kupunguza maumivu ya magoti, kumbi ni uzito umeongezeka unachotakiwa ni kupunguza
uzito na kuwa na staili inayokubalika unapokaa kwenye kiti ambayo haiyatesi
magoti unapokaa (yaani kupeleka mzigo/presha kwenye magoti) hivo na kuwa
salama.
Au
kuna wengine wanaumwa kiuna kwa sababu ya kutojua jinsi ya kuinua mzigo (kama
dumu la maji n,k) yaani akae mtindo gani anapuinua mzigo, nikimaanisha egemeo
lielekee wapi anapoinua mzigo.
Somo
ni SIKU ZOTE PENDA KUTUMIA UZOEFU WAKO ambao unaona unakupa matokeo mazuri,
kama tulivyojifunza kwa Daudi alitumia uzoefu wake na kumshinda Goliathi. Ila
usiache kujifunza na kukataa kila uzoefu/yaani kile unachofundishwa.Ila kila
kitu unachofundishwa kipime-Daudi alipima ndio maana alipokea yale mavazi ya
kivita lakini akaona mazito akaachana nayo.
www.mtibora.blogspot.com
Comments
Post a Comment