Skip to main content

FAIDA LUKUKI UNAZOPATA UNAPOOMBA KILA SIKU. (WHY DAILY PRAYER IS IMPORTANT)

Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa-Luka 18:1.

i-Unapoomba, ahadi za Mungu alizoziahidi kwako zinatimia.

Mungu aliahidi atatutupa Roho mtakatifu, lakini Roho mtakatifu alishuka kwa mitume wakiwa katika kuomba siku kumi.

Sehemu nyingine Mungu anasema huwapa thawabu wale wamtafutao. Unapoomba upo katika kitendo cha kumtafuta Mungu, kwa hiyo kuna vitu vingine vizuri huwa anakupa ukiwa unaomba hata kama hujaviomba.

Kwa hiyo kama huombi hupati ahadi zako.Kwani shetani anakua na nguvu ya kuzivuruga na kuleta vikwazo.

Waebrania 11: 6 – “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”.

 

ii-Unapoomba ni sawa na binadamu anavyohema kwa kuvuta hewa safi (oxygen) na kutoa nje hewa chafu (cabon), ukiomba unavuta paradiso ndani yako na kutoa nje heeee Dunia, au unamvuta Yesu ndani na kutuoa nje heee ubinadamu.Sasa unapoomba kila siku Yesu anazidi kujaa ndani yako na ubinadamu unakwisha ambao ndio huwapelekea watu kuingia majaribuni na kumtenda Mungu dhambi.

Neno linasema “Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni, roho i radhi ila mwili ni dhaifu”-Marko 14:38.

 

Hakikisha maombi yako unaomba kwa bidii na kwa moyo wako wote (Intensity prayer).Unapoomba kidogo unapewa maisha ya Yesu kidogo ndani yako.Ukiomba sana unamiminiwa maisha ya Yesu marefu ndani yako, sasa inabidi uchochee kila siku.Unapoocha kuomba Yesu anaoondoka unaingia majaribuni na kumtenda Mungu dhambi, ambacho ni kitu kibaya sana, kinaitwa kuanguka.

Neno linasema “Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai”-Waebrania 10:31.

 

Mungu atafanya kazi na wewe kama utaomba kwa bidii, hapo ndio panaitwa penye kulipa gharama (to pay the price). Mungu hawezi kukupa vitu vikubwa kama hulipi gharama kwa kuomba kwa muda mrefu na kwa moyo wote (Intesity prayer). Mungu anataka uwe na muda wa kutosha wa kukaa nae kupitia maombi.

 

iii-Unapoomba unamfanya shetani awe dhaifu sana.

Shetani ukiomba ni dhaifu sana hatakuweza. Ila usipoomba shetani ana nguvu sana sana sana atakuweza na kukutumikisha sana.

Ukiomba unafunga mlango shetani asiingie, ila usipoomba unamfungulia mwenyewe shetani mlango. Kama utamfungulia shetani mlango kwa kutokuomba maana yake uko hatarini, muda wowote tegemea kupatwa na mabaya wewe mwenyewe, familia yako, kazi yako, shule yako n.k

 

iv-Unapoomba unajazwa Roho mtakatifu.

Tunajazwa roho mtakatifu kila siku tunapoomba. Unapoacha kuomba kuna hatari roho mtakatifu akakuacha.Tunakuwa na uwezo wa kushinda dhambi tunapokuwa waombaji ni kwa sababu roho mtakatifu anayetuwezesha anakua amejaa ndani yetu kupitia hayo maombi.

Roho mtakatifu ni wa muhimu sana ndani yetu kwa sababu ana kazi nyingi kama;-

Kutuongoza, kutuponya magonjwa, kufanya uzalisha na uendelevu wa shughuli zetu, kutufanya tuwe na uwezo wa kuwaambie wengine habari njema, kuwavuta kwa Mungu n.k. 

Maombi na roho mtakatifu ni vitu vinavyotegemeana-Maombi yanapelekea kuwepo kwa Roho mtakatifu - na Roho mtakatifu anapelekea maombi mazito (Intensity prayer)

Luka 11:13 – “Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?

 

Angalizo-Omba usikate tamaa (prayers without faint)

Kama unamuombea mtoto wako, mke au mume n.k omba bila kukata tamaa, kwani maombi yako yanakusanywa ipo siku utapata muujiza wako, unachoomba kitafanikiwa.Lakini ukiombea jambo muda mrefu siku unapoocha na muujiza wako unapotea.

 

v-Unapoomba unafanya Malaika katika ulimwengu wako wa roho wakupiganie.

Malaika wapo kukutumikia wewe, unapoomba unakuwa kama unawaamrisha kufanya kazi, ukiacha kuomba wanaacha kufanya kazi hivyo kupelekea ulimwengu wako wa roho kushambuliwa na shetani. Kumbuka kitu chako chochote kinaanzia kwenye ulimwengu wa roho, kama kwenye ulimwengu wako wa roho hakuna ulinzi basi vitu vyako vitaharibiwa na vingine vitapolwa hutaviona kabisa katika macho ya kimwili.

Kumbuka Musa alipokua anainua mikono wakati wa vita walikuwa wakiwapiga maadui zao na aliposhusha walipigwa. Maana yake alipoinua mikono mambo yalitendeka katika ulimwengu wa roho na kupelekea kuwadhoofisha maadui zao.

Na wewe inua mikono yako, fanya maombi ya muda mrefu na kwa moyo wote (Intensity prayer) Mungu atafanya kwako mambo ya ajabu, makubwa na ya kutisha. Lipia gharama sasa (pay the price) hakikisha unaomba kila siku na kwa muda mrefu.

www.mtibora.blogspot.com

 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

SHARTI LILILOJIFICHA KWA AJILI YA UPONYAJI WA MWILI WAKO.

  Mungu anataka kukuponya lakini ili akuponye shariti lake ni hili; (Warumi 8: 11…Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu)   Unaona sharti hilo- ameanza na neno “Lakini, ikiwa” maana yake hilo ni sharti yaani ukiwa na Roho aliyemfufua Kristo Yesu yaani Roho wa Mungu au Roho mtakatifu ndani yako ndio utapata uponyaji kamili. Lakini kinyume chake hakuna uponyaji.   Sasa kumbe unahitaji kujua utampataje huyo Roho Mtakatifu na kumtunza kwa faida ya Roho na Mwili wako. Maana yake kama hauna huyo uko hatarini. (i)Tubu dhambi zako zote kwa Mungu-Maana Roho mtakatifu anataka awe yeye mwenyewe tu ndani yako. Moyo wako uwe kama karatasi nyeupe isiyokuwa na doa. (ii)Anza kuishi maisha ya kitakatifu kama kutokua na na chuki, kujiinua, hasira, woga, hofu, dharau, kuwaza mambo mabaya yaliyopi...

KITU KINACHOMUATHIRI BINADAMU KUTOFIKIA MALENGO YAKE.

Nyumba hujengwa kwa hekima (methali 24:3a) Hapa tunajifunza chocote kinachojengwa ili kifanikiwe kinahitaji Hekima, Bila Hekima chochote hakiwezi jengeka vizuri bali kitakuwa kinaharibiwa. Hapa nakuonyesha vitu vichache ambavyo unavijenga ili vifanikiwe vinahitaji Hekima; -Unajenga ndoa (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga watoto wako wawe wacha Mungu, pia wawe watu wazima wajitegemee na wawe msaada katika taifa (Inahitaji Hekima bila hiyo wanaharibika) -Unajenga kampuni, taasisi, biashara, kikundi, kazi, nchi (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga ujirani mwema (Inahitaji Hekima bila hiyo unaharibika) -Unajenga afya yako(Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Kumjenga au kumfundisha mtu kunataka hekima-bila hivyo utamvuruga kabisa. Hiyo ni mifano ya vitu vichache-lakini kumbuka chochote unachofanya unajenga na kinahitaji hekima. Hekima ni muhimu sana katika maisha yetu, mfalme Sulemani alipoambiwa na Mungu omba chochote aliomba Hekima....