(Mithali 4:23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima).Moyo wako ndio chanzo cha uzima/maisha/life.Kama ni maji ndio chanzo cha maji hakitakiwi kuchafuliwa.Hivyo moyo wako unatakiwa kuulinda kuliko chochote (fedha,magari n.k).Ukiruhusu mabaya katika moyo unakua umeharibu uzima wa kila kitu kama ndoa,afya,uzima wa roho n.k. Mabaya unayaruhusu vipi ndani ya moyo wako, ni kwa kuyatafakari/kuyawaza hapo unakua hujalinda moyo bali unakua umeingiza sumu kama kunywa maji ya betri.Moyo umeumbiwa kutafakari mambo mazuri tu, yenye sifa, tena yasiyokuumiza. Kwa kutafakari mambo mabaya yanayoleta chuki,hasira,kuhuzunika, kusononeka,kutosamehe,mambo yakupelekea kutenda dhambi-yamesababisha binadamu kupata magonjwa ya kimwili kabisa kwa sababu chazo cha uzima (Moyo) kimechafuliwa hivyo kimekuja kinyume cha uzima yaani mauti.Mfano wa kawaida hasira huleta maradhi ya pumu, kansa, kujiua n.k lakini pia unakosa uzima wa milele. (WAFILIPI 4:8 Hatimaye, ndug...