Skip to main content

ADUI ZAKO NI WA NYUMBANI MWAKO

Watu wengi wameathiriwa na wengine kuuawa na jamaa wa karibu kama mume, mke, watoto, majirani,wafanyakazi wenzako n.k

Mathayo 10: 36 “na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake”.
Jifunze kuwatambua, kuwaombea na jinsi ya kujikinga.
Somo hili linakupa mwanga kutambua na kujitambua, huenda Sehemu nyingine ulitumika kama adui na kuumiza au kuua wengi bila kujijua.

Neno kutoka Mithali 4:23 linasema “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima”
Maana yake kulinda Moyo ni kutoruhusu chochote kukuumiza moyo, utakaporuhusu basi chemchem zako za uzima unaziharibu na kutengeneza mauti.Ndio maana unakuta mtu kwa kuwaza sana anaumwa au anapatwa na mauti kabisa.Kwa hiyo mtu yoyote anayepenyeza kitu kitakachokuumiza katika moyo wako huyo ni adui. Anakuwa adui kwa sababu shetani ndio kumtumia, ila unatakiwa umpende, umuombee na usiruhusu mshale huo kukaa moyoni.Shetani huwatumia watu wa karibu kufanya uharibifu.
Tambua kuanzia sasa, mume, mke, watoto, ndugu, jirani, wafanyakazi na jamaa wa karibu wanaweza ongea jambo au kufanya matendo yanayoweza kupelekea moyo wako kuumia, kitendo cha kuumia moyo maana yake unapoteza uzima (wa mwili na roho). Ndio maana tunaambiwa tulinde sana moyo, yaani hayo yatakapokuja usikubali kuumia.
1.Kwa hiyo kuna wazazi wengine wameuawa na watoto wao, kwa kuona tabia mbaya za watoto wao wameumia mpaka kufa.Na sehemu nyingine watoto wamelia sana msibani, ila hawajui wao ndio wamewauwa wazazi wao.Kwani walipokua wanafanya matendo mabaya walikua wanashambulia mioyo ya wazazi wao na kuondoa chemchem ya uzima na kuleta mauti.

2.Sehemu nyingine wenzi katika ndoa wameuana au kuumizana/kuleta magonjwa kwa majibishano ya maneno magumu, kwa kufanya hivyo jua unaondoa uhai.Tena mwingine anatafuta neno gumu ili mwenzake aumie vizuri, maana yake hapo ndio unampiga tofali kubwa la kichwa unamuumiza moyo na kupelekea kufa taratibu. Ndio maana watu wengi ni wagonjwa sababu ya kupigana kwa maneno magumu, uzima umeondoka sasa watu wanayumba kama walevu. Magomvi ni majibishano ya maneno yanayoumiza kupelekea kuondoa uzima, kwani magomvi ni vita ambayo mtu hatoki damu ila anabunguliwa ndani taratibu, naweza kusema magomvi ni sumu anayonyweshwa mtu alafu anakwenda kufia mbele, hakuna ushahidi. Ewe mwanamke, usimjibu mumeo vibaya kwani utamuua kwa maneno yako bila kujua na utalia sana msibani. Inasemakana wakinamama ndio mabingwa wa maneno magumu, wazungu wanaita sharp words au sharp tongue au visu, ulimi wa kisu.

3.Mfanyakazi mwenzako, jirani au ndugu anaweza kukufanyia jambo likakuumiza. Anaweza kukusingizia, kukusema vibaya, hata kukutukana, sehemu nyingine mnaweza tukanana, jua hapo mnashambuliana sana rohoni na ndio uchawi huo, sehemu nyingine uchawi si kukalia kibuyu tu. Kwa sababu mnapojibishana vibaya kila mtu anatafuta neno la kumuumiza mwenzake, basi mmoja kama hana nguvu akipokea maneno hayo na kukaa moyoni basi uzima unatoweka anakufa, asipokufa kabisa basi anakua ameumizwa sana kama vile kukatwa miguu, au kutobolewa macho, tumbo n.k.

Kuanzia sasa hakikisha humuumizi mtu yoyote duniani kwa matendo au maneno yako, unapofanya hivyo jua shetani amekuingia na anakutumia wewe kama chumbo chake kuua mtu kiroho, kimwili, kiuchumi, kuua ndoa n.k.
Kwani uzima unapoondoka unaondoka katika nyanja zote.
Sasa uwe makini sana na mtu aliyekaribu yako,usijiachie, uwe na tahadhari sana.
Yesu alikuwa na tahadhari alimjua mwanafuzi atakae msaliti (Yuda) pia alimjua Petro alipoingiliwa na shetani.
Mathayo 16:23 “Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu”

Jinsi ya kushinda
Waefeso 6:16 “zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu”.

Imani ni ngao itakusaidia kukinga hiyo mishale inayochoma moyo wako na kuondoa uzima wako wa kimwili na kiroho.
-Imani utaipata kwa kusoma neno biblia - neno linasema imani chanzo chake ni kusikia ambako huja kwa neno la Mungu.
Pia neno linasema mtu hataishi kwa mkate tu bali kwa neno la Mungu, kama unakula chakula tu alafu husomi neno la Mungu kumbe huwezi kuishi kwa sababu mishale ya mwovu itakuchoma na kukuua.
-Imani pia utaipata kwa kuomba-Wanafuzi wa Yesu walipoambiwa wasemehe hata saba mala sabini wakasema “Bwana tuongezee Imani”

Kwa hiyo tumeona namna gani shetani anaweza kumtumia mtu wa karibu akawa adui, na namna gani shetani anaweza kukutumia.
Kuanzia sasa usitukane mtu, au usiongee jambo la kumuumiza mtu, kwa kufanya hivyo jua shetani amekufanya chombo chake kurusha mishale ya moto.

Tambua mamilioni ya watu Duniani wanaumia kupitia watu wa karibu, mtu wa mbali hawezi kukuumiza, kwani hakujui na yuko mbali hawezi kukufikia.
Mathayo 10: 36 “na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake”.

Leo Mungu amekuonyesha, chukua tahadhari, pia sehemu nyingine ulitumika kama adui.
Sasa tubu kwa Mungu na usirudie ili upone zije nyakati za burudani.


Comments

Popular posts from this blog

FAIDA LUKUKI UNAZOPATA UNAPOOMBA KILA SIKU. (WHY DAILY PRAYER IS IMPORTANT)

Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa-Luka 18:1. i-Unapoomba, ahadi za Mungu alizoziahidi kwako zinatimia. Mungu aliahidi atatutupa Roho mtakatifu, lakini Roho mtakatifu alishuka kwa mitume wakiwa katika kuomba siku kumi. Sehemu nyingine Mungu anasema huwapa thawabu wale wamtafutao. Unapoomba upo katika kitendo cha kumtafuta Mungu, kwa hiyo kuna vitu vingine vizuri huwa anakupa ukiwa unaomba hata kama hujaviomba. Kwa hiyo kama huombi hupati ahadi zako.Kwani shetani anakua na nguvu ya kuzivuruga na kuleta vikwazo. Waebrania 11: 6 – “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”.   ii-Unapoomba ni sawa na binadamu anavyohema kwa kuvuta hewa safi (oxygen) na kutoa nje hewa chafu (cabon), ukiomba unavuta paradiso ndani yako na kutoa nje heeee Dunia, au unamvuta Yesu ndani na kutuoa nje heee ubinadamu.Sasa unapoomba kila siku Yesu

SHARTI LILILOJIFICHA KWA AJILI YA UPONYAJI WA MWILI WAKO.

  Mungu anataka kukuponya lakini ili akuponye shariti lake ni hili; (Warumi 8: 11…Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu)   Unaona sharti hilo- ameanza na neno “Lakini, ikiwa” maana yake hilo ni sharti yaani ukiwa na Roho aliyemfufua Kristo Yesu yaani Roho wa Mungu au Roho mtakatifu ndani yako ndio utapata uponyaji kamili. Lakini kinyume chake hakuna uponyaji.   Sasa kumbe unahitaji kujua utampataje huyo Roho Mtakatifu na kumtunza kwa faida ya Roho na Mwili wako. Maana yake kama hauna huyo uko hatarini. (i)Tubu dhambi zako zote kwa Mungu-Maana Roho mtakatifu anataka awe yeye mwenyewe tu ndani yako. Moyo wako uwe kama karatasi nyeupe isiyokuwa na doa. (ii)Anza kuishi maisha ya kitakatifu kama kutokua na na chuki, kujiinua, hasira, woga, hofu, dharau, kuwaza mambo mabaya yaliyopita au uliyoten

KITU KINACHOMUATHIRI BINADAMU KUTOFIKIA MALENGO YAKE.

Nyumba hujengwa kwa hekima (methali 24:3a) Hapa tunajifunza chocote kinachojengwa ili kifanikiwe kinahitaji Hekima, Bila Hekima chochote hakiwezi jengeka vizuri bali kitakuwa kinaharibiwa. Hapa nakuonyesha vitu vichache ambavyo unavijenga ili vifanikiwe vinahitaji Hekima; -Unajenga ndoa (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga watoto wako wawe wacha Mungu, pia wawe watu wazima wajitegemee na wawe msaada katika taifa (Inahitaji Hekima bila hiyo wanaharibika) -Unajenga kampuni, taasisi, biashara, kikundi, kazi, nchi (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga ujirani mwema (Inahitaji Hekima bila hiyo unaharibika) -Unajenga afya yako(Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Kumjenga au kumfundisha mtu kunataka hekima-bila hivyo utamvuruga kabisa. Hiyo ni mifano ya vitu vichache-lakini kumbuka chochote unachofanya unajenga na kinahitaji hekima. Hekima ni muhimu sana katika maisha yetu, mfalme Sulemani alipoambiwa na Mungu omba chochote aliomba Hekima.