Skip to main content

UNAMWANGAMIZA UMPENDAYE BILA KUJUA.


Usimwambie rafiki yako au mke au mume wako habari zinazoweza kumfanya akajenga chuki juu ya upande mwingine, kwani utakuwa umemjengea kikwazo na wewe utakuwa umejijengea kikwazo,hata  ikiwa mume au mke wako amesemwa vibaya wewe ukajua usimwambie, unapomwambia huku ukifikiri ndio unampenda jua unamwangamiza.Kwani chuki atakayojenga hujui lini itakwisha, kwa sababu chuki ni pepo, basi litaalika mapepo mengine na kupelekea huyo umpendaye kuzidi kujenga tabia mbaya nyingine ambazo hata wewe uliyempelekea habari, tabia hizo zitakuzuru. Maana kupitia pepo la chuki lililo pandikzwa ndani yake, laweza leta pepo la wizi, pepo la uzinzi, pepo la ulevi, pepo la uchoyo n.k ambayo mapepo hayo yatakuzuru wewe uliyepeleka habari ukifikiri ni upendo kumbe unamuangamiza ndugu yako aliyekuwa hana hatia.tunajifunza kuwa habari zozote zinazoweza ibua chuki juu ya upande mwingine usimwambie nduguyu kwani unampanda pepo la chuki, pia tusijihusishe katika mambo ya uchonganishi kwani hicho nacho ni kitendo cha upandaji wa mapepo. Sasa kama nahusika kupanda watu mapepo mimi nitaitwa nani.Somo ni katika hali ya kupeana mwanga na kujitambua katika nia nzuri, kwani watu wengi hawakujua na kwa kutokujua, Mungu alijifanya kama haoni.

Waraka wa kwanza wa yohana 2:11 "Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho".










Comments

Popular posts from this blog

FAIDA LUKUKI UNAZOPATA UNAPOOMBA KILA SIKU. (WHY DAILY PRAYER IS IMPORTANT)

Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa-Luka 18:1. i-Unapoomba, ahadi za Mungu alizoziahidi kwako zinatimia. Mungu aliahidi atatutupa Roho mtakatifu, lakini Roho mtakatifu alishuka kwa mitume wakiwa katika kuomba siku kumi. Sehemu nyingine Mungu anasema huwapa thawabu wale wamtafutao. Unapoomba upo katika kitendo cha kumtafuta Mungu, kwa hiyo kuna vitu vingine vizuri huwa anakupa ukiwa unaomba hata kama hujaviomba. Kwa hiyo kama huombi hupati ahadi zako.Kwani shetani anakua na nguvu ya kuzivuruga na kuleta vikwazo. Waebrania 11: 6 – “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”.   ii-Unapoomba ni sawa na binadamu anavyohema kwa kuvuta hewa safi (oxygen) na kutoa nje hewa chafu (cabon), ukiomba unavuta paradiso ndani yako na kutoa nje heeee Dunia, au unamvuta Yesu ndani na kutuoa nje heee ubinadamu.Sasa unapoomba kila siku Y...

KITU KINACHOMUATHIRI BINADAMU KUTOFIKIA MALENGO YAKE.

Nyumba hujengwa kwa hekima (methali 24:3a) Hapa tunajifunza chocote kinachojengwa ili kifanikiwe kinahitaji Hekima, Bila Hekima chochote hakiwezi jengeka vizuri bali kitakuwa kinaharibiwa. Hapa nakuonyesha vitu vichache ambavyo unavijenga ili vifanikiwe vinahitaji Hekima; -Unajenga ndoa (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga watoto wako wawe wacha Mungu, pia wawe watu wazima wajitegemee na wawe msaada katika taifa (Inahitaji Hekima bila hiyo wanaharibika) -Unajenga kampuni, taasisi, biashara, kikundi, kazi, nchi (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga ujirani mwema (Inahitaji Hekima bila hiyo unaharibika) -Unajenga afya yako(Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Kumjenga au kumfundisha mtu kunataka hekima-bila hivyo utamvuruga kabisa. Hiyo ni mifano ya vitu vichache-lakini kumbuka chochote unachofanya unajenga na kinahitaji hekima. Hekima ni muhimu sana katika maisha yetu, mfalme Sulemani alipoambiwa na Mungu omba chochote aliomba Hekima....

SIKU ZOTE PENDA KUTUMIA UZOEFU WAKO.

Daudi alikua kijana mdogo lakini alimuua Goriathi jitu kubwa lililowasumbua sana ndugu zake.Wakati anakwenda kupigana nalo watu wake walimdharau na kuona hawezi.Alipong’ang’ania walimvalisha mavazi yao ya vita, lakini yeye aliyavua akaenda kupambana na goriathi kwa kutumia uzoefu wake, Daudi alitumia kombeo na kweli aliweza kumuangamiza goriathi aliyesumbua sana. Kujifunza ni vizuri lakini changanya na uzoefu wako. -Tumia uzoefu wako katika kuendesha ndoa yako japo umeona unaleta matunda ya kuishi vizuri kwa upendo, umoja na amani. Watu wengi ndoa zao zimeharibiwa kwa kutumia uzoefu wa wengine. Unaweza ambiwa wanaume hawafai au wanawake hawafai kumbe wa kwako anafaa. Mfano- mtu mume wake anaposafiri au mke wake anaposafiri anaweza ambiwa na watu wengine kuwa huko mume wako au mke wako alipo atakua si salama anafanya uasherati-hapo anakuwa anapewa uzoefu na watu wengine ambao sio sahihi. Sasa unakuta shuku mbaya zinamuingia mtu na kuleta chuki kati yao. -Hata katika ulaji kuna ...