Skip to main content

MAISHA/UZIMA/MAMBO YAKO YOTE YAPO HAPA

(Mithali 4:23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima).Moyo wako ndio chanzo cha uzima/maisha/life.Kama ni maji ndio chanzo cha maji hakitakiwi kuchafuliwa.Hivyo moyo wako unatakiwa kuulinda kuliko chochote (fedha,magari n.k).Ukiruhusu mabaya katika moyo unakua umeharibu uzima wa kila kitu kama ndoa,afya,uzima wa roho n.k.
Mabaya unayaruhusu vipi ndani ya moyo wako, ni kwa kuyatafakari/kuyawaza hapo unakua hujalinda moyo bali unakua umeingiza sumu kama kunywa maji ya betri.Moyo umeumbiwa kutafakari mambo mazuri tu, yenye sifa, tena yasiyokuumiza.
Kwa kutafakari mambo mabaya yanayoleta chuki,hasira,kuhuzunika, kusononeka,kutosamehe,mambo yakupelekea kutenda dhambi-yamesababisha binadamu kupata magonjwa ya kimwili kabisa kwa sababu chazo cha uzima (Moyo) kimechafuliwa hivyo kimekuja kinyume cha uzima yaani mauti.Mfano wa kawaida hasira huleta maradhi ya pumu, kansa, kujiua n.k lakini pia unakosa uzima wa milele.
(WAFILIPI 4:8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo) Moyo umeumbwa kutafakari vitu kama vilivyoelezwa hapo juu.ukitafakari kinyume na hapo unakuwa unachafua chanzo chako cha uzima na kuleta kinyume cha uzima yaani mauti.

(Proverbs 4: 23 And keep watch over your heart with all care; so you will have life.)

Anza sasa kufanya DIET ya mawazo kama watu wanavyofanya diet ya chakula ili wawe na afya nzuri kuna baadhi ya vyakula wanaacha.Kwa hiyo na wewe kila wazo sio la kuwaza.na wewe ambaye umekuwa na mawazo mengi ya kukuumiza yaliyotokana na watoto,mume,mke,ndugu,mali na kadhalika kuanzia sasa usielekee kuwaza mawazo hayo, utashangaa mawazo hayo yaletayo machungu yataanza kuishiwa nguvu pole pole na kupotea.(Kwa kufanya hivyo tunaita unakuwa unajiscan kama computer inavyo scan virus au unakuwa unaondoa sumu moyoni kwenye chanzo chako cha LIFE/MAISHA UZIMA.
Moyo pia hautakiwi kuwaza/kutafakari mawazo ya kukupeleke kutenda dhambi kama uzinzi,ulevi,kutukana,kupigana n.k kwani utakuwa unaukosa uzima wa roho wa Milele.
Kuanzia sasa anza kukwepa vitu vitakavyopelea moyo kuwaza mabaya.Kimbiza macho yako kuangalia vitu vibaya, Kimbiza masikio yako kusikiliza vitu vibaya, kwani mazungumzo mabaya huaribu tabia.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA LUKUKI UNAZOPATA UNAPOOMBA KILA SIKU. (WHY DAILY PRAYER IS IMPORTANT)

Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa-Luka 18:1. i-Unapoomba, ahadi za Mungu alizoziahidi kwako zinatimia. Mungu aliahidi atatutupa Roho mtakatifu, lakini Roho mtakatifu alishuka kwa mitume wakiwa katika kuomba siku kumi. Sehemu nyingine Mungu anasema huwapa thawabu wale wamtafutao. Unapoomba upo katika kitendo cha kumtafuta Mungu, kwa hiyo kuna vitu vingine vizuri huwa anakupa ukiwa unaomba hata kama hujaviomba. Kwa hiyo kama huombi hupati ahadi zako.Kwani shetani anakua na nguvu ya kuzivuruga na kuleta vikwazo. Waebrania 11: 6 – “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”.   ii-Unapoomba ni sawa na binadamu anavyohema kwa kuvuta hewa safi (oxygen) na kutoa nje hewa chafu (cabon), ukiomba unavuta paradiso ndani yako na kutoa nje heeee Dunia, au unamvuta Yesu ndani na kutuoa nje heee ubinadamu.Sasa unapoomba kila siku Yesu

SHARTI LILILOJIFICHA KWA AJILI YA UPONYAJI WA MWILI WAKO.

  Mungu anataka kukuponya lakini ili akuponye shariti lake ni hili; (Warumi 8: 11…Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu)   Unaona sharti hilo- ameanza na neno “Lakini, ikiwa” maana yake hilo ni sharti yaani ukiwa na Roho aliyemfufua Kristo Yesu yaani Roho wa Mungu au Roho mtakatifu ndani yako ndio utapata uponyaji kamili. Lakini kinyume chake hakuna uponyaji.   Sasa kumbe unahitaji kujua utampataje huyo Roho Mtakatifu na kumtunza kwa faida ya Roho na Mwili wako. Maana yake kama hauna huyo uko hatarini. (i)Tubu dhambi zako zote kwa Mungu-Maana Roho mtakatifu anataka awe yeye mwenyewe tu ndani yako. Moyo wako uwe kama karatasi nyeupe isiyokuwa na doa. (ii)Anza kuishi maisha ya kitakatifu kama kutokua na na chuki, kujiinua, hasira, woga, hofu, dharau, kuwaza mambo mabaya yaliyopita au uliyoten

KITU KINACHOMUATHIRI BINADAMU KUTOFIKIA MALENGO YAKE.

Nyumba hujengwa kwa hekima (methali 24:3a) Hapa tunajifunza chocote kinachojengwa ili kifanikiwe kinahitaji Hekima, Bila Hekima chochote hakiwezi jengeka vizuri bali kitakuwa kinaharibiwa. Hapa nakuonyesha vitu vichache ambavyo unavijenga ili vifanikiwe vinahitaji Hekima; -Unajenga ndoa (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga watoto wako wawe wacha Mungu, pia wawe watu wazima wajitegemee na wawe msaada katika taifa (Inahitaji Hekima bila hiyo wanaharibika) -Unajenga kampuni, taasisi, biashara, kikundi, kazi, nchi (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga ujirani mwema (Inahitaji Hekima bila hiyo unaharibika) -Unajenga afya yako(Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Kumjenga au kumfundisha mtu kunataka hekima-bila hivyo utamvuruga kabisa. Hiyo ni mifano ya vitu vichache-lakini kumbuka chochote unachofanya unajenga na kinahitaji hekima. Hekima ni muhimu sana katika maisha yetu, mfalme Sulemani alipoambiwa na Mungu omba chochote aliomba Hekima.