TUKISEMA YESU AMEKUOKOA
AU MTU HUYU ANAKWENDA MBINGUNI maana yake ameokolewa MAWAZO yake, kuwa
makini na kitu hiki.Mtu aliyeokolewa na Yesu mfumo wa mawazo yake
hubadilika.Mtu huyu Mawazo yake/ tafakari zake zote lazima zijikite kwenye UPENDO, UZIMA na HAKI kwa sababu hivo vitu
ndio nia ya Mungu.Shetani nia yake ni kinyume cha UPENDO,UZIMA na HAKI yaani
yeye amejikita kwenye CHUKI,MAUTI na UOVU. Kuanzia sasa anza kupima mawazo
yako, unamuwazia nini raisi,nchi yako, nchi nyingine, balozi, mke wako, mume
wako, mfanyakazi mwenzako, bosi wako, muumini mwenzako, mchungaji wako,
mfanyabiashara mwenzako, n.k
Hata kama watu hawa wamekufanyia mabaya wewe unatakiwa watu
hawa uwawazie UPENDO, UZIMA na HAKI, kwa maana hiyo watu hawa watukula matunda
ya vitu hivyo kutoka kwako, kwani vitu hivyo UPENDO, UZIMA na HAKI hutoa
matunda haviishii kusimama vyenyewe kwenye mawazo yako.
HATARI- ni hii watu wengi wanamuabudu Mungu lakini mfumo wa
MAWAZO yao bado haujaokolewa.Mtu anamuabudu/ anamcha Mungu lakini bado anamuwazia vibaya raisi wake, nchi yake,
mbunge wake,balozi wake, bosi wake, mchungaji wake, muumini mwenzake n.k Hii
haitakusaidia.
Basi tengeneza rafiki YANGU.
Sikiliza rafiki yangu unaweza ukawa unafanya matendo
mema,ila kama bunge lako la MAWAZO muda wote halijajikita kwenye UPENDO,UZIMA
na HAKI hatari bado ipo, Muombe Mungu
akutengeneze huku nawe ukifanyia mazoezi swala la kushinda Mawazo mabaya.
Sehemu nyingine yatakuja mawazo mabaya, usikate tamaa ukaona
umeharibika, hapo Mungu anachotaka usikubaliane na mawazo hayo mabaya, pambana
nayo Mungu atakusaidia utashinda, hiyo ni moja ya vita ya kiroho.
Neno linasema hata
nitoe mali na mwili wangu uungue moto kama sina Upendo hainisaidii kitu.
PIA Neno linasema – “ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na
kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu” yeye atasema ondokeni
siwajui.
Angalia hatari hii Hawa wanaoambiwa (SIWAJUI) ni watu
waliokua wanajishugulisha na Mungu ila MAWAZO yao yalikua hayajaokolewa. Kwa
hiyo ndugu zangu tutende mema huku tukiyaangalia sana MAWAZO yetu tunayowaza kutwa
nzima, je yanampendeza Mungu.
Kumbuka YESU anaokoa MAWAZO yako, kwa maana hiyo ndio MBEGU
ya kila kitu.
2 wakoritho 10:5
5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho
juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
1 Wakoritho 13-3
1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina
upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa
yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina
upendo, si kitu mimi.
3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena
nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.
(Maana yake mtu anaweza kufanya mambo hayo hapo juu huku
MAWAZO yake hayajaokolewa-maana kama mtu hana UPENDO huyo mawazo yake yako
kinyume na nia ya MUNGU ambayo ni UPENDO, UZIMA na HAKI. Kuanzia sasa kila
jambo utakololiwazia, liangalie kwa sura ya kulitendea UPENDO, UZIMA na HAKI)
Luka 13:26-28a
26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako,
nawe ulifundisha katika njia zetu.
27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu
ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.
28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno,
Comments
Post a Comment