Mauti na Uzima vi
kinywani mwako.
Mithali 18:21
21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao
waupendao watakula matunda yake.
Mara nyingi binadamu amejiloga mwenyewe kwa kutumia ulimi
wake vibaya
Kujitamkia maneno mabaya. Mfano mimi mjinga, mimi
msahaulifu, mimi mbovu n.k
Kuanzia sasa tumia ulimi vizuri kujitamkia mema ili ule
matunda yake, sema mimi nimebarikiwa, moyo wangu ni mzima, figo zangu ni nzima,
afya yangu haina matatizo, watoto wangu wamebarikiwa, mimi nina akili, mimi
nina kumbukumbu n.k penda kujitamkia
maneno haya mara kwa mara.
Sehemu nyingine mwanadamu amelogwa kwa kudanganywa, mfano
Ugonjwa huu hautibiki, mwanamke nyoka, ndoa ndoano n.k kwa kudaganywa huku mtu
mwingine amejikuta akiamini na kutamka, basi inakua kama anavyotamka. Wengine
wamekua wakisema, wewe unataka kuingia kwenye ndoa, sisi tunataka kutoka bwana.
Sasa hali hii imekua ikimuaminisha mtu mwingine na
kutamka.Kumbe hao waliokumbana na ugumu wa jambo hilo ilikuwa kwa ajili ya
matatizo yao wenyewe, sasa wamekua wakiwaaminisha hata watu ambao hawana
matatizo na na watu hao wamekua wakiamini na kutamka hivyo nao kupelekea kupata
matatizo yanayofanana.
Kwa hiyo watu wenye mazoea/experience mbaya wanawapandikiza
vitu potofu
Watu wengine.
Kuna rafiki yangu alikua kusoma nchi za nje, alimuacha mke
wake Tanzania, sasa wanafunzi aliokutana nao huku wanaotoka nchi nyingine
kutoka Afrika, nao wameacha wake zao nchini kwao, wakawa wanamshauri rafiki
yangu kutembea/kufanya uzinzi na wanawake wengine wakimuaminisha kuwa wanawake
si waaminifu kwa hiyo mke wake hawezi kumsubiri, nae anatembea na wanaume
wengine huko aliko.
Sasa huo ni mfano halisi ya jinsi watu wenye uzoefu
mbaya/bad experience wanataka kuaaminisha matatizo yaliyowatokea kuwa ni hali
ya ujumla, usipokua makini unaweza amini na kuharibu mambo yako. Sasa hivi
ndivyo binadamu alivyodanganywa katika mambo mengine mengi, kutoka kwa watu
wenye uzoefu mbaya/watu waliokumbana na mambo mabaya kutokana na tabia zao
mbaya wenyewe.
Ukweli wa maneno ni sawa na MBEGU njema, lakini adui
amewavizia watu wengi amepanda MAGUGU yaani amepotosha ukweli wa neno.mfano
badala ya kusema ndoa ni kitu chema, sasa watu wanasema ndoa ngumu ni kama
ukuta mkubwa ambao watu wanatamani watoke wanashindwa.
Angalia neno hapo chini;
Mathayo 13:24-25
24 Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni
umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake;
25 lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu
katikati ya ngano, akaenda zake.
Kuanzia sasa usiseme;
-Usiseme wanawake nyoka, utapata matatizo kwenye ndoa
yako.Neno linasema mke ni msaidizi tena ni zawadi kutoka kwa Mungu.
-Usiseme ndoa ngumu,Neno linaona ndoa ni njema ni kanisa na
iheshimiwe.
-Usiseme ugonjwa huu umeshindikana, neno (mbegu njema)
inasema hakuna linaloshindikana kwa Mungu.
-Usiseme mtoto huyu ameshindikana. neno (mbegu njema)
inasema hakunalina loshindikana kwa Mungu. Kazi yako ni kumtamkie mototo mema ili
ale matunda ya ulimi wako.
-Usiseme vyuma vimekaza utakwama kweli. Neno linasema
huendelea toka nguvu hata nguvu, maana yake hakuna kukwama wala kudumaa, mambo
yanavyozidi kuwa magumu wewe utaendelea juu tu. Mfano enzi za Nuhu, nchi ilivyozidi
kujaa maji watu wanakufa Nuhu ndivyo alivyozidi kwenda juu na safina.
-Uwe makini kutumia kinywa na uwe makini katika mazungumzo.
Mtu anaweza kukulaani bila yeye kujua. Mfano bahati mbaya mwanzoni mwa mwaka mtu
anaugua, rafiki yake anakuja kumpa pole kwa nia nzuri, anasema pole rafiki
yangu huu mwaka mbaya kwako, inabidi usikubali, usiseme asante, sema hapo hapo
kwa upendo "nafuta usemi wako kwa damu ya Yesu"
Sasa tumeangalia sehemu chache ila ziko nyingi.
Unaona hapo chini, tumia kinywa vizuri.
Mithali 18:7
7 Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake, Na midomo yake ni
mtego wa nafsi yake.
Comments
Post a Comment