Skip to main content

Usiwe Mti unao haribu Ardhi.


Binadamu aliyefanikiwa ni mtu ambaye ni msaada katika jamii iliyomzunguka.
Mtu wa namna hii anafananishwa na Mti unaozaa matunda.
Katika jamii zetu kuna makundi mbali mbali yanahitaji msaada, sehemu nyingine sio fedha ni mawazo tu na kuwatia moyo.
Hatari ni hii-kama wewe ni mtu mzuri wa maadili, unajilinda sana/msafi sana, hutendi dhambi, ila unajiishia mwenyewe na familia yako, husaidii watu wenye shida unafananishwa na mti ambao upo lakini hauzai matunda. Hatari ni kwamba unaonekana ni mti ambao unabana nafasi na pia unaharibu ardhi.
(LUKA 13:7 Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu?)
Binadamu ni mfanao wa miti ya aina tatu.
-Mti wa kwanza ni ule unaozaa matunda mazuri (yaani huyu ni yule mtu ambaye hatendi dhambi ni msafi na anasaidia jamii iliyomzunguka, watu wanafaidika kutoka kwake. Huyu ana Heri)
 -Mti wa pili ni ule unaozaa matunda mabaya (Mtu huyu huwafanyia watu wengine mambo mabaya ya kuwaumiza kama kuwatukana, kuwaibia, kuwasenginya, kuwaua n.k. watu hawafaidiki na lolote kutoka kwake bali ni maumivu tu, Mtu huyu ni mtenda dhambi. Mtu wa jinsi hii Ole imesimama kwake)
-Mti wa tatu upo unaonekana lakini hauzai matunda (yaani huyu ni mtu anajilinda na dhambi lakini hajishughulishi kwa ajili ya wengine, anahesabika hazai matunda. Mtu wa jinsi hii yuko hatarini asipobadadilka na kuanza kuwatendea wengine mema,kuzaa matunda kama neno linavyosema hapo juu LUKA 13:7)

Yesu atakapokuja kuhukumu ataangalia matendo mema uliyowatendea wengine
Mathayo 25:34-45
34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;
35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;
36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.
37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?
38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?
39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?
40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;
43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.
44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?
45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.

Sasa ni muda wako wa kuzaa matunda.
Mfano kuna vijana katika eneo lako wapo vijiweni-Sasa ilitakiwa wewe mwenye maadili, msomi na mwenye uwezo kuwatembelea vijana hao siku moja moja, sio kukaa peke yako na kuishia kuwasema tu (wavuta bangi wale, waizi wale). Inatakiwa kutoka na kuongea nao kwa upendo kuwaelekeza wanatakiwa kufanya nini waweze kusonga mbele. Kwa kufanya hivyo unatawatia nguvu na kuwaonyesha maisha mengine mazuri.Vijana wengi wanaingia vijiweni na kukosa makaka wazuri wakuwaelekeza maisha, sasa tunawaachia makaka wabaya wanawapokea na wanawaelekeza kuvuta bangi na kuiba.Tunawaachia makaka wabaya wanawaonyesha maisha mabaya na vijana kuona HAYA NDIO MAISHA ya kuvuta bangi, kuiba, kwenda jela na kutoka.
Wewe kwa kwenda wanapokuona tu, kuna kitu unawavuvia wanaanza kutamani maisha yako yanayo kubalika, wanatamani kuwa kama wewe.
Unaweza ukawa kwa upande wako huwezi kuanza kuwaingia, watafutie watu wenye uwezo huo, watafutie program/programme/project za kuwasogeza mbele, fanya wewe kuwa kiunganishi kati yao na fursa mbalimbali unazoweza kuziona na kuwaunganisha. Sehemu nyingine huenda unakumbana na fursa zao ila hufanyi connection/uunganishi wowote unaziacha zinawapita.
Pia kuna wasichana katika eneo lako wanahitaji msaada wa mawazo mazuri hata fedha kwa ajili ya mitaji midogo midogo, ni kazi yako wewe dada/ kaka/baba/mama kuwasaidia. Usiwaachie watu wabaya kuwaelekeza vijana wetu maisha mabaya. Sasa ni muda wewe kuwa URGENT OF CHANGE katika jamii yako.
Onyesha thamani yako kwa kufanya mabadiliko katika jamii yako.Usiishie kwenda kazini na baaada ya kurudi nyumbani na kujifungia ndani.
Anza kidodogo kwani Mungu anapenda tujishughulishe kwa ajili ya wengine.

Mungu amekubariki na kukufundisha maadili yake si kwa ajili yako peke yako kwani atakudai. Tumia chochote alichokupa Mungu kiwafaidishe na wengine.
Yapo makundi mengi katika jamii yanayohitaji msaada, mimi nimetoa mfano mmoja wa vijana tu.

Mtu aliyefanikiwa ni yule aliye BUILD HIS PERSONALITY AND IMPACT THE WORLD (aliyejijengea uwezo na kuleta mabadiliko chanya ulimwenguni). Sasa sio lazima uguse ulimwengu wote, fanya kwa kadri ya uwezo wako.
 Kama una mali na hufanyi chochote katika jamii iliyokuzunguka, wewe hujafanikiwa.

Angalizo-Ukisaidia jamii huku wewe unatenda dhambi, bado haikusaidii, inakua sawa na kumpa Mungu rushwa, yeye hapokei rushwa. Inatakiwa vitu viwili viende pamoja (yaani usitende dhambi na saidia jamii iliyokuzunguka)
Anza sasa- zaa Matunda.
Be Fruitful 




Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

FAIDA LUKUKI UNAZOPATA UNAPOOMBA KILA SIKU. (WHY DAILY PRAYER IS IMPORTANT)

Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa-Luka 18:1. i-Unapoomba, ahadi za Mungu alizoziahidi kwako zinatimia. Mungu aliahidi atatutupa Roho mtakatifu, lakini Roho mtakatifu alishuka kwa mitume wakiwa katika kuomba siku kumi. Sehemu nyingine Mungu anasema huwapa thawabu wale wamtafutao. Unapoomba upo katika kitendo cha kumtafuta Mungu, kwa hiyo kuna vitu vingine vizuri huwa anakupa ukiwa unaomba hata kama hujaviomba. Kwa hiyo kama huombi hupati ahadi zako.Kwani shetani anakua na nguvu ya kuzivuruga na kuleta vikwazo. Waebrania 11: 6 – “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”.   ii-Unapoomba ni sawa na binadamu anavyohema kwa kuvuta hewa safi (oxygen) na kutoa nje hewa chafu (cabon), ukiomba unavuta paradiso ndani yako na kutoa nje heeee Dunia, au unamvuta Yesu ndani na kutuoa nje heee ubinadamu.Sasa unapoomba kila siku Y...

KITU KINACHOMUATHIRI BINADAMU KUTOFIKIA MALENGO YAKE.

Nyumba hujengwa kwa hekima (methali 24:3a) Hapa tunajifunza chocote kinachojengwa ili kifanikiwe kinahitaji Hekima, Bila Hekima chochote hakiwezi jengeka vizuri bali kitakuwa kinaharibiwa. Hapa nakuonyesha vitu vichache ambavyo unavijenga ili vifanikiwe vinahitaji Hekima; -Unajenga ndoa (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga watoto wako wawe wacha Mungu, pia wawe watu wazima wajitegemee na wawe msaada katika taifa (Inahitaji Hekima bila hiyo wanaharibika) -Unajenga kampuni, taasisi, biashara, kikundi, kazi, nchi (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga ujirani mwema (Inahitaji Hekima bila hiyo unaharibika) -Unajenga afya yako(Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Kumjenga au kumfundisha mtu kunataka hekima-bila hivyo utamvuruga kabisa. Hiyo ni mifano ya vitu vichache-lakini kumbuka chochote unachofanya unajenga na kinahitaji hekima. Hekima ni muhimu sana katika maisha yetu, mfalme Sulemani alipoambiwa na Mungu omba chochote aliomba Hekima....

SIKU ZOTE PENDA KUTUMIA UZOEFU WAKO.

Daudi alikua kijana mdogo lakini alimuua Goriathi jitu kubwa lililowasumbua sana ndugu zake.Wakati anakwenda kupigana nalo watu wake walimdharau na kuona hawezi.Alipong’ang’ania walimvalisha mavazi yao ya vita, lakini yeye aliyavua akaenda kupambana na goriathi kwa kutumia uzoefu wake, Daudi alitumia kombeo na kweli aliweza kumuangamiza goriathi aliyesumbua sana. Kujifunza ni vizuri lakini changanya na uzoefu wako. -Tumia uzoefu wako katika kuendesha ndoa yako japo umeona unaleta matunda ya kuishi vizuri kwa upendo, umoja na amani. Watu wengi ndoa zao zimeharibiwa kwa kutumia uzoefu wa wengine. Unaweza ambiwa wanaume hawafai au wanawake hawafai kumbe wa kwako anafaa. Mfano- mtu mume wake anaposafiri au mke wake anaposafiri anaweza ambiwa na watu wengine kuwa huko mume wako au mke wako alipo atakua si salama anafanya uasherati-hapo anakuwa anapewa uzoefu na watu wengine ambao sio sahihi. Sasa unakuta shuku mbaya zinamuingia mtu na kuleta chuki kati yao. -Hata katika ulaji kuna ...