Shetani anachofanya unapokosea anakujengea hukumu na kukuonyesha hufai
kwa MUNGU. Ni kweli dhamili tunazo zinatuonyesha tunapokosea tunatubu,
tunajirekebisha na kuamini Baba MUNGU ametusamehe, na kweli tunasamehewa Kweli.
MUNGU ametuagiza mtu anapokukosea tumsamehe hata saba mara sabini kwa siku
moja, maana yake hata wewe ukimkosea MUNGU saba mara sabini kwa siku moja
atakusamehe.
Watu wengi wakikosea shetani huzungumza nao mfululizo
kuwaambia hujasamehewa ili awachukue, na kweli wengi wanazidi kushuka na kudondosha vitu
mkononi walivyopewa na MUNGU na wengine anawateka kabisa.
SHETANI AKIKUZUNGUMZISHA KUANZIA SASA KUWA HUJASAMEHEWA, MWAMBIE
KWENDA ZAKO MIMI NI MTOTO WA MUNGU, atakuachia.
Chapa mwendo ila usifanye dhambi makusudi, unapokosa tubu
hapo hapo usisubiri kutubu ukifika nyumbani au usiku wakati wa maombi yako kwani hujui saa ya kuondoka Duniani. MUNGU
anakusikia ukiomba ukiwa unatembea, unaendesha gari au unafaya kazi na
kadhalika.
MUNGU anakupenda sana
na anajishughulisha sana na wewe, kama vile tunavyojishughulisha na watoto wetu
wanaposumbua, unakuta kafukuzwa shule hii kwa tabia mbaya unampeleka shule
nyingine na Mungu ni vile vile.
Adamu na Hawa walipotenda dhambi na uwepo wa Mungu kuwatoka
wakawa uchi, tazama japo wamemuuzi Mungu lakini Mungu akaua mnyama akawafunika
kwa ngozi ya mnyama ili wasiwe uchi, bado watu wakazidi kutenda dhambi na
kumuuzi MUNGU lakini bado akashuka Dunia kupitia Yesu akauawa kwa ajili yako
ili kufanya mambo yako yawe mazuri na uwe na uzima wa milele, analeta Agano
jipya.
1 Yohana 2:1-2
1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende
dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo
mwenye haki,
2 naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi
zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.
www.mtibora.blogspot.com
Comments
Post a Comment