Skip to main content

Vitu vinavyofanya Mungu asisikie maombi yako


Vitu vinavyofanya mungu asisikie maombi yako.hivo hapo chini.Jitahidi kuvifanya vyote ili mungu akusikie na kukutendea.
1-Kuomba tutumie kwa tamaa zetu.Yakobo 4:3
( Yakobo 4:3- Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu).
Kumbe naweza omba Imani, vitu vingine vya kimungu, na mahitaji ya kimwili vibaya, pale ninapopenda nionekane na wanadamu na pia vitu hivyo visiwe msaada kwa wengine.
2-Maovu na dhambi-Isaya 59:1-2
"1 Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;
2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia".

3-Kuvitwaa vinyago na kuviweka moyoni Ezekiel 14:3 
(Ezekiel 14:3 Mwanadamu, watu hawa wametwaa vinyago vyao na kuvitia mioyoni mwao, nao wameweka kwazo la uovu wao mbele ya nyuso zao. Je! Ni laiki yangu niulizwe na wao katika neno lo lote?) Kuweka moyoni kinyago ni kupenda kitu zaidi ya Mungu kama mke, watoto, kazi, shule n.k

4-Kutosikiliza kilio cha maskini.Mithali 21:13
"13 Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini, Yeye naye atalia, lakini hatasikiwa".

5-Kutosamehe Marko 11:25 
(Marko 11:25 Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu). Maana usiposamehe Mungu hakusamei dhambi naye hasikii wenye dhambi.
6-Mahusiano mabaya kati ya mume na mke.1 Petro 3:7
(1 petro 3:7 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe).
 7-Kutokuamini Yakobo 1:5-7
"6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana".

8- Kutokaa ndani ya Yesu na kutoshika maneno yake  (Yohana 15:7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa).Kushika maneno maana yake kuyajua na kuyatenda.

9- Kuomba bila kutumia jinan laYesu.
 (Yohana 14:13-14
13 Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.)

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA LUKUKI UNAZOPATA UNAPOOMBA KILA SIKU. (WHY DAILY PRAYER IS IMPORTANT)

Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa-Luka 18:1. i-Unapoomba, ahadi za Mungu alizoziahidi kwako zinatimia. Mungu aliahidi atatutupa Roho mtakatifu, lakini Roho mtakatifu alishuka kwa mitume wakiwa katika kuomba siku kumi. Sehemu nyingine Mungu anasema huwapa thawabu wale wamtafutao. Unapoomba upo katika kitendo cha kumtafuta Mungu, kwa hiyo kuna vitu vingine vizuri huwa anakupa ukiwa unaomba hata kama hujaviomba. Kwa hiyo kama huombi hupati ahadi zako.Kwani shetani anakua na nguvu ya kuzivuruga na kuleta vikwazo. Waebrania 11: 6 – “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”.   ii-Unapoomba ni sawa na binadamu anavyohema kwa kuvuta hewa safi (oxygen) na kutoa nje hewa chafu (cabon), ukiomba unavuta paradiso ndani yako na kutoa nje heeee Dunia, au unamvuta Yesu ndani na kutuoa nje heee ubinadamu.Sasa unapoomba kila siku Y...

SHARTI LILILOJIFICHA KWA AJILI YA UPONYAJI WA MWILI WAKO.

  Mungu anataka kukuponya lakini ili akuponye shariti lake ni hili; (Warumi 8: 11…Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu)   Unaona sharti hilo- ameanza na neno “Lakini, ikiwa” maana yake hilo ni sharti yaani ukiwa na Roho aliyemfufua Kristo Yesu yaani Roho wa Mungu au Roho mtakatifu ndani yako ndio utapata uponyaji kamili. Lakini kinyume chake hakuna uponyaji.   Sasa kumbe unahitaji kujua utampataje huyo Roho Mtakatifu na kumtunza kwa faida ya Roho na Mwili wako. Maana yake kama hauna huyo uko hatarini. (i)Tubu dhambi zako zote kwa Mungu-Maana Roho mtakatifu anataka awe yeye mwenyewe tu ndani yako. Moyo wako uwe kama karatasi nyeupe isiyokuwa na doa. (ii)Anza kuishi maisha ya kitakatifu kama kutokua na na chuki, kujiinua, hasira, woga, hofu, dharau, kuwaza mambo mabaya yaliyopi...

KITU KINACHOMUATHIRI BINADAMU KUTOFIKIA MALENGO YAKE.

Nyumba hujengwa kwa hekima (methali 24:3a) Hapa tunajifunza chocote kinachojengwa ili kifanikiwe kinahitaji Hekima, Bila Hekima chochote hakiwezi jengeka vizuri bali kitakuwa kinaharibiwa. Hapa nakuonyesha vitu vichache ambavyo unavijenga ili vifanikiwe vinahitaji Hekima; -Unajenga ndoa (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga watoto wako wawe wacha Mungu, pia wawe watu wazima wajitegemee na wawe msaada katika taifa (Inahitaji Hekima bila hiyo wanaharibika) -Unajenga kampuni, taasisi, biashara, kikundi, kazi, nchi (Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Unajenga ujirani mwema (Inahitaji Hekima bila hiyo unaharibika) -Unajenga afya yako(Inahitaji Hekima bila hiyo inaharibika) -Kumjenga au kumfundisha mtu kunataka hekima-bila hivyo utamvuruga kabisa. Hiyo ni mifano ya vitu vichache-lakini kumbuka chochote unachofanya unajenga na kinahitaji hekima. Hekima ni muhimu sana katika maisha yetu, mfalme Sulemani alipoambiwa na Mungu omba chochote aliomba Hekima....