Jinsi unavyofanya diet ya chakula, yaani unaacha baadhi ya
vyakula unavyojua vitahatarisha afya yako.Basi vivyo hivyo fanya diet ya mawazo,
mawazo yote unayowaza na kuona yanaumiza moyo usiwaze.uwe kama jongoo ambae
hana macho ukigusa kijiti anageuza.nawe ukiona kuna jambo ukiwaza linakuumiza
usielekee huko, yaani usiendelee kuliwaza.utashangaa jambo hilo linalo kuumiza
linaishiwa nguvu kwa kutoliwaza na linakwisha.Mfano ndugu yako anaweza
akakusingizia jambo baya n.k
Mbili tusiishi maisha ya kukubali moyo wetu ujeruhiwe.Ukijeruhika
unajipanga mara moja usikae hapo muda mrefu.Kujipanga ni kuacha kuwaza mpaka
sumu yote inaisha.anza kuwa na mpango wa kuondoa sumu mawazo yote yanayokuumiza
na kuwa free.Hiyo inaitwa unajiscan mwenyewe kama computer.unajiscan mpaka moyo
unakuwa free from virus, usibebe jambo lolote la kukuumiza.utaweza kwa kukimbia
kuacha kuwaza basi mambo hayo yataanza kuishiwa nguvu mpaka yanakwisha kabisa.
Comments
Post a Comment