Jinsi unavyofanya diet ya chakula, yaani unaacha baadhi ya
vyakula unavyojua vitahatarisha afya yako.basi vivyo hivyo fanya diet ya
mawazo, mawazo yote unayowaza na kuona yanaumiza moyo usiwaze. Uwe kama jongoo
ambae hana macho akigusa kijiti anageuza.Ukiona kuna jambo ukiliwaza
linakuumiza usielekee huko, yaani usiendelee kuliwaza. Jambo hilo linalo
kuumiza utashangaa linaishiwa nguvu kwa kutoliwaza na linakwisha.Mfano ndugu
yako anaweza akakusingizia jambo baya, mtoto wako akawa anaenda visivyo,
migogoro kazini, au umefiwa n.k.kuacha kuwaza mambo yanayojeruhi moyo ndio kunaitwa
kuscan moyo kama computer.Uwe na program ya kujiscan.Usikubali kuishi na moyo
wako ukiwa umejeruhika kwani huwezi kuleta matokea muzuri/best katika maisha
yako.Moyo ukijeruhika huwezi kupata maona mazuri, huwezi kuelewa kitu chochote
katika kiwango cha juu, huwezi kufanya kazi au biashara katika kiwango cha juu,
huwezi kumcha mungu katika kiwango cha juu.
Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa-Luka 18:1. i-Unapoomba, ahadi za Mungu alizoziahidi kwako zinatimia. Mungu aliahidi atatutupa Roho mtakatifu, lakini Roho mtakatifu alishuka kwa mitume wakiwa katika kuomba siku kumi. Sehemu nyingine Mungu anasema huwapa thawabu wale wamtafutao. Unapoomba upo katika kitendo cha kumtafuta Mungu, kwa hiyo kuna vitu vingine vizuri huwa anakupa ukiwa unaomba hata kama hujaviomba. Kwa hiyo kama huombi hupati ahadi zako.Kwani shetani anakua na nguvu ya kuzivuruga na kuleta vikwazo. Waebrania 11: 6 – “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”. ii-Unapoomba ni sawa na binadamu anavyohema kwa kuvuta hewa safi (oxygen) na kutoa nje hewa chafu (cabon), ukiomba unavuta paradiso ndani yako na kutoa nje heeee Dunia, au unamvuta Yesu ndani na kutuoa nje heee ubinadamu.Sasa unapoomba kila siku Y...
Comments
Post a Comment