Mambo yote yaliyokatazwa na kanuni ya dunia ukifanya
unaharibu ustawi wako. kila kitu kina kanuni, ukikosea kanuni hupati matunda
tarajiwa. Kupika kuna kanuni, kula, kujenga nyumba,kulima, kuoga, kuendesha
gari n.k
je wajua kanuni ya kuendesha maisha?
Mambo yote yaliyokatazwa yana madhara, hatujakatazwa kama
tunacheza mchezo/game na aliyeyakataza, hapana amekataza sababu ya madhara kutoka ktk jambo husika.
Mfano aliyetengeneza sumu ya wadudu na kukataza binadamu
asitumie kama kunywa, si kwamba anacheza game na wewe ni kwamba ukinywa unapata
madhara kweli.
Mfano wa vitu vilivyokatazwa na madhara yake katika ustawi
wako:-
(I)POMBE-Inaharibu- akili,mahusiano, utendaji kazi, muonekano
wa mwili unakuwa mbaya, inaharibu afya, mapato yanapotea kwa kitu kisicho na
maana katika familia, ulevi unaondoa uaminifu wako na kutoaminika, maamuzi
yasiyo na busara ukali ukali tu, uvivu, kupungua kwa nguvu za mwili, maradhi TB
Presha, ajali inahusika, ulemavu, uasherati, kukosa amani ambayo ni kitu cha
msingi katika maisha yako ukikosa amani hata uwe na mali nyingi kwako ni
sifuri.hofu na mashaka,kifo n.k
(II)UZINZI/UASHERATI – Unaharibu akili, mzinzi hana akili
ndio kanuni ya dunia hutuambia, Maradhi, Kuharibu mahusiano katika familia na
kupelekea kuharibu ustawi wa familia na future ya watoto, kuzaa watoto
wasiotarajiwa hivyo kukosa matunzo na kuwa na taifa la watu wabaya baadae
watakao jihusisha na ujambazi, ukatili, uvunjaji wa amani/haki na mauaji hata
kushawishika kuingia katika vikundi vibaya, wivu, Ugomvi, mauaji, kukosa amani
ambayo ni kitu cha msingi katika maisha yako ukikosa amani hata uwe na mali
nyingi kwako ni sifuri, hofu na mashaka, utendaji wa kazi chini ya kiwango,
PENZI KITOFU CHA UZEMBE, Kifo n.k
(III)HASIRA -Inaleta magonjwa katika mwili wako kama Presha,
kansa, mauaji, muonekano mbaya wa mwili/uso unakunjamana, kualibu ustawi wa
familia na watoto, malezi chini ya kiwango, maamuzi mabaya hasira hasira tu,
utendaji wa kazi chini ya kiwango, maono/idea chini ya kiwango, ajali, hasira
hukaa kwa mpumbavu hiyo ndio kanuni ya dunia yatwambia, kukosa amani ambayo ni
kitu cha msingi katika maisha yako ukikosa amani hata uwe na mali nyingi kwako
ni sifuri.hofu na mashaka,kifo n.k
(IV)UCHAFU-Kuharibu afya yako, kutokubalika, kuharibi
mahusiano kona zote, muonekano mbaya, maradhi,kushusha ufanisi wa biashara,
kupoteza wateja, kukosa amani ambayo ni kitu cha msingi katika maisha yako
ukikosa amani hata uwe na mali nyingi kwako ni sifuri.hofu na mashaka,kifo n.k
(V)CHUKI- Inaleta magonjwa katika mwili wako kama Presha,
kansa, mauaji, muonekano mbaya wa mwili/uso unakunjamana, kualibu ustawi wa
familia na watoto, malezi chini ya kiwango, maamuzi mabaya, utendaji wa kazi
chini ya kiwango, upendeleo bila kujali tija, maono/idea chini ya kiwango,
ajali, hasira hukaa kwa wapumbavu, kukosa amani ambayo ni kitu cha msingi
katika maisha yako ukikosa amani hata uwe na mali nyingi kwako ni sifuri.hofu
na mashaka,kifo n.k
(VI)FITINA, UONGO, UZUSHI, MASENGENYO –huleta magomvi,
mauaji, chuki,kutokubalika, kuharibu mahusiano pale inapogundulika umehusika,
na lazima utangundulika sababu kanuni ya dunia inasema siri zote zitawekwa
wazi.
kukosa amani ambayo ni kitu cha msingi katika maisha yako
ukikosa amani hata uwe na mali nyingi kwako ni sifuri.hofu, mashaka,kifo n.k
Hiyo ni mifano ya vitu vichache vilivyokatazwa – endelea
kutafakari athari za makatazo mengine kama; wizi,ushirikina (kwenda kwa waganga
wa kienyeji)
Kujivuna kujiona bora kuliko wengine,ufisadi, rushwa,
uchawi, wivu,ubakaji
ulawiti, ufiraji, ulafi, sigara na Mengine.
Vitu hivyo ulivyovipima unaonaje, vina faida?
Unapofanya jambo moja kati ya yaliyokatazwa jua umeisha
jiumiza/kuharibu ustawi wako.
Unapoliludia hilo hilo moja unaendelea kujiumiza/kuharibu
ustawi wako.
Unapofanya lingine baya jua umeendelea kujiumiza/ kuharibu
ustawi wako.
Comments
Post a Comment