Fikra potofu ni mawazo yoyote yanayokushawishi
kufanya kitu kibaya, mfano kutoongea na mtu fulani,
kumchukia mtu, jirani yako au mfanyakazi mwenzako, mwanafunzi mwenzako,
kuiba, kumpiga mtu, kutukana, kuua, kujiua, kudanganya,
kusaliti, kuzini, kulewa, kuvuta bangi, n.k.
Jinsi ya kushinda fikra potofu ni kuzikataa, fikra potofu
yoyote iambie nakukataa, alafu usiendelee kuwaza kuelekea huko (mfano fikra inakushawishi kumchukia jirani
yako/mafanyakazi /mwanafunzi/mfugaji/ au mfanyabishara mwenzako kwa sababu
amekukosea, fikra iambie nakukataa, alafu iambie mimi natakiwa kumpenda jirani
yangu hata adui yangu na pia kumsamehe anaye nikosea)
Fikra potofu yoyote ni roho mbaya/roho mbaya maana yake ni
roho ya shetani. Fikra potofu au roho mbaya au roho ya shetani usikubaliane
nayo kwa kutenda inavyokuelekeza/kukusukuma.Ukikubaliana nayo basi roho hiyo ya
shetani hukutawala na kuwa ajenti wa shetani. Roho hiyo itakua inakusukuma
kufanya vitu vingi potofu mfano wa vichache nilivyoeleza hapo juu, huo ndio
uajenti wa shetani.
Fikra potofu tabia yake kuu ni kuharibu/destroy upande wa
pili alafu kuja kukuharibu na wewe pia, sababu unachotenda unajipandia wewe
mwenyewe siku zote hukurudia.dunia ni duara, unachotenda huzunguka kukurudia
wewe.
Angalizo:Fikra potofu waweza kupewa kupitia mtu mwingine katika
maongezi, mtu anaweza ongea ubaya wa mtu Fulani ukajikuta na wewe unamchukia. Jitahidi
kuwa makini na watu unaokutana nao au marafiki.
Swali la kirafiki:wewe umeisha wahi kumpanda mtu fikra
potofu/mawazo mabaya/roho mbaya, yaani roho ya shetani.
Kama umewahi fanya hivyo, basi tubu kwa Mungu na usirudie
tena.
Comments
Post a Comment