Kama bidhaa inavyojengewa ubora, hata wewe waweza kujijengea ubora, njia ni
hii waza mambo mazuri na kujizoeza kuyafanyia kazi.Mawazo ni mbegu zinazokua na
kuzaa tabia.Chanzo cha tabia fulani ni mawazo yako, au mawazo unayopewa na
kukubaliana kutoka upande wa pili,hii ni kanuni ya dunia.kuanzia sasa anza
kuwaza mawazo mazuri kama kuwapenda watu na kuwafanyia mema, waza kuwa jamii
niifanyie nini jema, waza kuwa mimi nataka niwe mtu wa kusamehe, waza kuwa mimi
nataka niwe jitu moja poleee/baridiii, waza kuwa katika kitengo nilichokuwepo
niwasaidie watu bila rushwa, waza kuwa nataka majirani zangu niwapende na
kuwasaidia.waza kuwa napenda mke au mume wangu nisimkwaze au kumsaliti
kabisa,waza napenda nikipata gari niwape watu lifti, waza napenda nikitukanwa
au kuambiwa neno la kuumiza mimi nisijibu pia kwa neno la kuumiza kama
kisu/sharp tongue n.k (ukiona uko kinyume na mfano wa mawazo hayo juu machache
juo ubora wako kama bidhaa uko chini sana)
Penda kuwaza mawazo mazuri na kujizoeza kuyatende itakuwa
tabia na utakuwa umejiongezea ubora. mtu atakapokuita jina lako na ubora wako
atauona kuwa mpole, mwaminifu, mwenye huruma, mwenye busara na hekima
n.k.haitakiwi jamii ikikuona ione ubaya kama mchelewaji,mvivu chapombe, dakika
mbili mbele, malaya,tapeli, mwizi, mzulumishi, mzee wa fitina, mgomvi, n.k.
unapojijingea ubora yale mazuri unayoyafanya ni mbegu kwako,
nawe utalipwa mazuri yale yale tena yoliyozidi.unavuna utakachopanda hiyo ni
kanuni ya dunia. jiulize unapanda nini sasa, unalofanya sasa lazima lazima
lazima likurudie mwenyewe.
Comments
Post a Comment